Posts

Kunenepa Kupita Kiasi Husababishwa na Nini?

“Tunakabili tatizo kubwa ambalo linaweza kuathiri sana afya ya watoto wetu. Hatua isipochukuliwa sasa ili kuzuia tatizo hilo, watu watazidi kunenepa kupita kiasi.”—William J. Klish, profesa wa magonjwa ya watoto. WATU fulani wasio na tatizo la kunenepa huwachambua watu walionenepa kupita kiasi na kuwaona kuwa wavivu na goigoi. Lakini je, kweli tatizo hilo ni dogo hivyo? Je, kunenepa kupita kiasi ni tatizo la watu wavivu wasiopenda kufanya mazoezi? Au je, mara nyingi tatizo hilo husababishwa na mambo makubwa ambayo ni vigumu kuyazuia? Je, Husababishwa na Urithi, Mazingira, au Yote Mawili? Kitabu  Food Fight  kinasema hivi: “Kwa muda mrefu watu wamejadili ikiwa kunenepa kupita kiasi husababishwa na urithi au mazingira.” Ni nini maana ya urithi katika habari hii? Wengine husema kwamba kwa kawaida mwili wa mwanadamu huhifadhi kalori za ziada kwa ajili ya mahitaji ya wakati ujao. Kitabu hicho kinaendelea kusema: “Kwa makumi ya miaka, uchunguzi umefanywa ili kugundua jinsi urit...

Magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu.

Image
Niliwahi soma habari moja iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania ikimkariri Dk. Ali Mzige akisema ‘afya za watanzani hatarini’. Nilishawishika kuisoma habari yote kwani alichokisema ndiyo hali halisi ambayo inahitaji kutiliwa msisitizo ili watu waelimike na wajue jinsi ya kujiepusha na hatari hiyo. Dk. Mzige, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya IMTU na Mtaalamu wa Afya ya Jamii , alisema kuwa magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu yanaongezeka nchini kwa kasi na inakadiriwa ifikapo mwaka 2020, magonjwa hayo yatachukua zaidi ya ailimia 70 ya magonjwa yote. Aidha, katika habari hiyo, Dk. Mzige alisema kuwa magonjwa hayo hujulikana pia kama ‘magonjwa ya kusendeka’ (chronic disease) ambayo hutokana na ulaji mwingi wa vyakula vya kusindika (processed food) na kuacha kula vyakula vya asili. Kwa kawaida, vyakula hivyo vya kusindika, au vya kwenye makopo kama vinavyojulikana, mara nyingi huwa na mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi, kemikali nyingi na viungo ba...

Athari za unene

Athari za unene uliopindukia ni kusababisha matatizo mengi ya kiafya. Kwa mtu mwenye tatizo la unene uliopitiliza huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa hatarishi kama hataweza kudhibiti tatizo kwa haraka. Madhara ya unene kupita kiasi huweza kuwa ni yale yanayoonekana  siku kwa siku au kupata magonjwa hatarishi. Matatizo ya siku kwa siku ya unene kupita kiasi: -Kupumua kwa shida -Kutokwa jasho kwingi -Kukoroma ukiwa umelala -Kushindwa kufanya shughuli za nguvu -Kujisikia mchovu mara kwa mara -Maumivu ya joint na mgongo -Kushindwa kujiamini na kutojikubali -Kujihisi umetengwa -Huweza pia kusababisha mfadhaiko Magonjwahatarishi yanayoweza kusababishwa na kuwa na unene uliopitiliza ni kama yafuatayo: - Kisukari aina ya 2 - High blood pressure - High cholestrol (lehemu nyingi) -Asthma - Kiharusi (Stroke) -Ugonjwa wa mishipa ya moyo (Coronary heart disease) -Aina tofauti za kansa kama vile kansa ya utumbo mpana,kansa ya matiti na kansa ya mfuko wa mimba - Mawe kwenye mfuko wa nyon...

Nguvu za kiume

Image
  Jua tatizo la nguvu za kiume Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote. Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME SIYO UGONJWA, ni DALILI YA UGONJWA. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake.  Kuna sababu zaidi ya 200 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume. Mtu aweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo?  Nguvu za kiume ni nini? Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo lenyewe.  Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume? Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50n...

Madini ya Zink na Ugumba

Image
UHUSIANO KATI YA UGUMBA NA UPUNGUFU WA MADINI YA ZINC   Zinc ni elementi muhimu mno katika afya ya binadamu hivi kwamba ukosefu kidogo unaweza kuleta madhara makubwa. Zinc ni ya muhimu sana kwa sababu inapatikana ndani ya kila kiungo cha mwili cha binadmu na inahusika kwa karibu sana na kugawanyika kwa seli za mwili. Ni antioxidant yenye nguvu sana, inayosaidia kuzuia kansa, na pia inahusika moja kwa moja katika ufanyaji kazi wa tezi mbalimbali za kutengeneza homoni na kuweka sawa viwango vya homoni katika mwili. Makadiridio yasiyo rasmi yanaonyesha kuwa asilimia 25 ya watu duniani wanakabiliwa na upungufu wa zinc na kwa sababu mwili wa binadamu hauhifadhi zinc, tunalazimika kupata zinc kila siku. VYANZO VYA MADINI YA ZINC Kwa msomaji wa makala hii, tambua kwamba huhutaji kwenda mbali zaidi kupata madini haya muhimu kwa afya yako, maana hupatikana kwenye vyalula vinavyotyuzunguka kiurahisi kama 1.maini 2. mboga za spinach 3. mbegu za maboga na karanga 4. nyama nyekundu 5. mah...

Kuvimba miguu

Tatizo la kuvimba miguu husababishwa na kujikusanya kwa majimaji ambayo uvuja kutoka katika mishipa ya damu kutokana na sababu mbalimbali zinazosababisha damu ishindwe kurudi kwenye moyo kutoka katika miguu. Hali hii huweza kutokea pia kwenye mapafu, ubongo, tumboni, na kwenye mapaja lakini kutokana na mvuto wa ardhi huweza kuonekana zaidi kwenye upande wa miguu na bila hata maumivu yeyote. Mambo yanayochangia na kusababisha tatizo ili mara nyingi huwa ni ujauzito, ama iwapo unaugua ugonjwa sugu wa ini, figo vilevile moyo unaposhindwa kufanya kazi yake na dawa za kudhibiti shinikizo la damu husababisha miguu kufura. Na pia kuna baadhi ya watu wanaposafiri kwa muda mrefmiguu yao huvimba. Hata hivyo kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kufanya ili kuisaidia miguu yako kwa hali ya kawaida lakini kwanza Muone daktari endapo kuvimba kwa miguu inaambatana na kubanwa na kifua, kushindwa kupumua, maumivu makali ya kifua, kuna maumivu au joto kali miguuni mwako, na kama una matatizo ya moyo, ini...

AINA ZA MAUMIVU YA TUMBO

Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ya mbavu kulia yanaweza kusababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo, maambukizi kwenye mfuko wa nyongo  Cholecystitis , uvimbe wa ini, jipu kwenye ini, saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo. Maumivu chini ya chembe ya moyo husababishwa na vidonda vya tumbo, kiungulia, saratani ya tumbo na saratani ya kongosho. Maumivu pembeni mwa kitovu husababishwa na mawe ya figo Kidney Stones, maambukizi ya figo, Pyelonephritis na  maambukizi kidoletumbo Acute Appendicitis Maumivu chini ya kitovu huweza kusababishwa na maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID, vivimbe vya mji wa uzazi, mimba kuharibika na saratani ya kibofu cha mkojo. Sababu nyingine za maumivu ya tumbo ni utumbo kujiziba Intestinal Obstruction,  utumbo kujisokota Volvulus, kula sumu na  mzio wa chakula fulani au ugonjwa wa Crohn Crohn’s Disease,  N...