Nguvu za kiume

Jua tatizo la nguvu za kiume Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote. Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME SIYO UGONJWA, ni DALILI YA UGONJWA. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake. Kuna sababu zaidi ya 200 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume. Mtu aweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo? Nguvu za kiume ni nini? Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo lenyewe. Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume? Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50n...