Athari za unene


Athari za unene uliopindukia ni kusababisha matatizo mengi ya kiafya. Kwa mtu mwenye tatizo la unene uliopitiliza huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa hatarishi kama hataweza kudhibiti tatizo kwa haraka. Madhara ya unene kupita kiasi huweza kuwa ni yale yanayoonekana  siku kwa siku au kupata magonjwa hatarishi.

Matatizo ya siku kwa siku ya unene kupita kiasi:

-Kupumua kwa shida

-Kutokwa jasho kwingi

-Kukoroma ukiwa umelala

-Kushindwa kufanya shughuli za nguvu

-Kujisikia mchovu mara kwa mara

-Maumivu ya joint na mgongo

-Kushindwa kujiamini na kutojikubali

-Kujihisi umetengwa

-Huweza pia kusababisha mfadhaiko

Magonjwahatarishi yanayoweza kusababishwa na kuwa na unene uliopitiliza ni kama yafuatayo:

-Kisukari aina ya 2

-High blood pressure

-High cholestrol (lehemu nyingi)

-Asthma

-Kiharusi (Stroke)

-Ugonjwa wa mishipa ya moyo (Coronary heart disease)

-Aina tofauti za kansa kama vile kansa ya utumbo mpana,kansa ya matiti na kansa ya mfuko wa mimba

-Mawe kwenye mfuko wa nyongo (gallstone)

-Ugonjwa wa maungio ya mifupa wa Osteoarthiritis

-Magonjwa ya ini

-Magonjwa ya figo

-Kisukari wakati wa ujauzito (gestational diabetes)

-Presha ya mwanamke wakati wa ujauzito (Pre-eclampsia)

Unene uliopitiliza huweza kupunguza urefu miaka ya kuishi kwa takribani miaka 3 hadi 10 kulingana na kiwango tatizo lilichofikia. Kwa Ulaya unene kupindukia unakadiriwa kusababisha kifo cha mtu 1 kati ya watu 13.

Suala la kupunguza uzito wa mwili sio mchezo. Linahitaji kujitolea na maamuzi thabiti na hufanya kazi vyema kama utakamilisha dozi au ratiba yote. Katika mada itakayofuata tutajadili jinsi ya kupunguza uzito au unene uliopitiliza.

Kama una swali,maoni au ushauri kuhusiana na mada hii,tafadhali usisite kutuandikia kupitia 
email: mputae84@gmail.com
            mputae0@gmail.com
Phone: +255625748804
              +255767962720
              +255717962720

Comments

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

Madini ya Zink na Ugumba