JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE AU WA KIUME

WANANDOA au hata wasio na ndoa hujiuliza maswali haya. Nini nifanye ili nipate mtoto wa kike au kiume? Je, kuna dawa au vyakula vya kusaidia kupata mtoto ninayemtaka? Siku gani nikikutana na mwenzangu naweza kupata mtoto wa kiume au kike? Jinsia ya mtoto Mtoto hutengenezwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la kike. Mbegu ya kiume hubeba vinasaba vya X na Y, wakati yai la mwanamke likiwa na vinasaba vya X peke. Ikikutana na mbegu ya kiume yenye kinasaba cha X na yai la kike (yenyewe yana vinasaba vya X peke yake) mtoto wa kike hutungwa. Mbegu ya kiume yenye kinasaba cha Y ikikutana na yai la kike, mtoto wa kiume hutungwa. Mbegu ya kiume Y + Yai la kike X = Mtoto wa Kiume. Mbegu ya kiume X + Yai la kike X = Mtoto wa Kike. Njia za Kupata Mtoto Wa Jinsia Uipendayo Mbegu za kiume zenye vinasaba vya Y huwa ni nyepesi, husafiri kwa haraka katika via vya uzazi vya mwanamke na huishi kwa muda mfupi ukilinganisha na mbegu zenye vinasaba X. Zenye vinasaba X huwa nzito za...