NETWORK MARKETING (BIASHARA YA MTANDAO)

IJUE BIASHARA YA MTANDAO(NETWORK MARKETING) NA FAIDA ZAKE. Nawasalimu Ndugu zangu na Kuwakaribisha katika ukurasa huu wa Forever Living Products. Naam karibuni sasa tushirikiane katika mada hapo juu. Wengi huenda sio mara ya kwanza kusikia juu ya biashara ya mtandao(Network Marketing). Kama tunaijua twendelee kuijua zaidi, na kwa wale ambao ndio Mara yao ya kwanza kusikia, basi tufuatane hadi mwisho wa makala hii ili tuijue, karibuni. Network Marketing(Biashara mtandao) ni biashara inayofanyika kwa kuwaunga zaidi watu kusambaza na kuuza bidhaa za kampuni kama wasambazaji ambao hulipwa kulingana na utendaji kazi wa mtu binafsi. Aina hii ya biashara huwa na kampuni linalozalisha bidhaa Fulani na kuziuza kwa kutumia wasambazaji waliokubaliwa na kampuni, ambapo wasambazaji hulipwa kamisheni kulingana na mauzo, lakini pia kupata faida fulani(retail profit) katika bidhaa hizo anapoziuza kwa mtumiaji wa mwisho. Hivyo msambazaji(distributor) anapouza zaidi ndipo kampuni nalo linapouza zaidi na...