Magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu.
Niliwahi soma habari moja iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania ikimkariri Dk. Ali Mzige akisema ‘afya za watanzani hatarini’. Nilishawishika kuisoma habari yote kwani alichokisema ndiyo hali halisi ambayo inahitaji kutiliwa msisitizo ili watu waelimike na wajue jinsi ya kujiepusha na hatari hiyo.
Dk. Mzige, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya IMTU na Mtaalamu wa Afya ya Jamii , alisema kuwa magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu yanaongezeka nchini kwa kasi na inakadiriwa ifikapo mwaka 2020, magonjwa hayo yatachukua zaidi ya ailimia 70 ya magonjwa yote.
Aidha, katika habari hiyo, Dk. Mzige alisema kuwa magonjwa hayo hujulikana pia kama ‘magonjwa ya kusendeka’ (chronic disease) ambayo hutokana na ulaji mwingi wa vyakula vya kusindika (processed food) na kuacha kula vyakula vya asili.
Kwa kawaida, vyakula hivyo vya kusindika, au vya kwenye makopo kama vinavyojulikana, mara nyingi huwa na mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi, kemikali nyingi na viungo bandia vingi.
Ulaji wa vyakula hivyo, humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na magonjwa sugu kama vile
- kisukari,
- shinikizo la damu na
- saratani.
Magonjwa haya hayampati mtu hadi pale anapoanza kuyatengeneza mwenyewe kutokana na tabia yake ya ulaji. Leo tulizungumze hili kwa mara nyingine.
Unajitengenezeaje magonjwa?
Nimependa kauli aliyoitumia Dk. Mzige isemayo ‘magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu’. Kwa wasioelewa usemi huu ningeomba kuwafafanulia kwani una maana sana. Tabia yako ya ulaji ndiyo inayozungumziwa hapa. Tangu unapoamka asubuhi unafanya nini na unakula nini, una kulaje, unalalaje, ndiko kunakoamua afya yako.
Kumbuka pia ule msemo wetu maarufu usemao, jinsi ulivyo ni kunatokana na unavyokula. Ukiwa na kitambi au kiribatumbo kunatokana na ulaji wako, ukiwa mnene, mwembamba, kumetokana na ulaji wako, ukiwa na ‘presha’ imetokana na ulaji wako, ukiwa na saratani imetokana na ulaji wako, n.k.
Kujua kwa kina juu ya afya wasiliana nami👇
mputae84@gmail.com
mputae0@gmail.com
+255625748804
+255767962720
Comments
Post a Comment