Kuvimba miguu
Tatizo la kuvimba miguu husababishwa na kujikusanya kwa majimaji ambayo uvuja kutoka katika mishipa ya damu kutokana na sababu mbalimbali zinazosababisha damu ishindwe kurudi kwenye moyo kutoka katika miguu.
Hali hii huweza kutokea pia kwenye mapafu, ubongo, tumboni, na kwenye mapaja lakini kutokana na mvuto wa ardhi huweza kuonekana zaidi kwenye upande wa miguu na bila hata maumivu yeyote.
Mambo yanayochangia na kusababisha tatizo ili mara nyingi huwa ni ujauzito, ama iwapo unaugua ugonjwa sugu wa ini, figo vilevile moyo unaposhindwa kufanya kazi yake na dawa za kudhibiti shinikizo la damu husababisha miguu kufura.
Na pia kuna baadhi ya watu wanaposafiri kwa muda mrefmiguu yao huvimba.
Hata hivyo kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kufanya ili kuisaidia miguu yako kwa hali ya kawaida lakini kwanza
Muone daktari endapo kuvimba kwa miguu inaambatana na kubanwa na kifua, kushindwa kupumua, maumivu makali ya kifua, kuna maumivu au joto kali miguuni mwako, na kama una matatizo ya moyo, ini na figo.
Lakini kama huna dalili hizo unaweza kufanya yafuatayo kujitibu mwenyewe nyumbani
• Kwanza fanya mazoezi kwa kuinua miguu yako juu kuelekea kwa upande wa kichwa na wakati umelala angalau kwa muda wa dakika 30 ili kuwezesha damu ya kutosha kurudi kwenye moyo.
• 2. Fanya hivi angalau mara 3 kwa siku kupata matokeo bora zaidi
• 3. Kufanya mazoezi laini pia itakusaidia kupeleka damu kwenye moyo na hivyo kurekebisha mzunguko wa damu
• 4. Wakati unasafiri safari ndefu hakikisha unasimama mara kwa mara.
• Epuka kuvaa kwa muda mrefu nguo zinazobana sehemu za mapaja.
• Na kama umnene kupita kiasi fanya mazoezi mara kwa mara ili kupunguza uzito
Wasiliana nami +255767962720/ +255625748804
Comments
Post a Comment