Madini ya Zink na Ugumba
UHUSIANO KATI YA UGUMBA NA UPUNGUFU WA MADINI YA ZINC
Zinc ni elementi muhimu mno katika afya ya binadamu hivi kwamba ukosefu kidogo unaweza kuleta madhara makubwa. Zinc ni ya muhimu sana kwa sababu inapatikana ndani ya kila kiungo cha mwili cha binadmu na inahusika kwa karibu sana na kugawanyika kwa seli za mwili. Ni antioxidant yenye nguvu sana, inayosaidia kuzuia kansa, na pia inahusika moja kwa moja katika ufanyaji kazi wa tezi mbalimbali za kutengeneza homoni na kuweka sawa viwango vya homoni katika mwili. Makadiridio yasiyo rasmi yanaonyesha kuwa asilimia 25 ya watu duniani wanakabiliwa na upungufu wa zinc na kwa sababu mwili wa binadamu hauhifadhi zinc, tunalazimika kupata zinc kila siku.
VYANZO VYA MADINI YA ZINC
Kwa msomaji wa makala hii, tambua kwamba huhutaji kwenda mbali zaidi kupata madini haya muhimu kwa afya yako, maana hupatikana kwenye vyalula vinavyotyuzunguka kiurahisi kama
1.maini
2. mboga za spinach
3. mbegu za maboga na karanga
4. nyama nyekundu
5. maharage na maziwa na
6. Uyoga na Parachichi
Baadhi ya dalili ambazo zitakusaidia kutambua kuwa una upungufu wa madini ya zinc ni pamoja na
Ø Kupoteza hamu ya kula
Ø Kujiskia vibaya na huna mood mara kwa mara
Ø Kupungua kwa uwezo wa kutambua ladha ama harufu ya kitu
Kama unatambua una dalili zote hizi hapo juu basi hakikisha unaonana na dactari wako ili uweze kupata vipimo na ushauri wa kitaalamu.
MADINI YA ZINC HUSAIDIA
1) Kusawazisha kiwango cha sukarikatika mwili
2) Kusaidia utengenezwaji wa protini kwenye mwili
3) Kusaidia kusapoti mfumo wa upumuaji
4) Kuongeza ufananyaji kazi wa seli za mwili
5) Kupunguza sumu mwilini na kusaidia mmengeyo wa chakula
UPUNGUFU ZA ZINC NA AFYA YA UZAZI
Upungufu wa zinc husababisha ugumba kwa jinsia zote, wanaume na wanawake na kuwasababishia tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango kidogo cha zinc katika mwili hukuza madhara ya msongo wa mawazo katika mwili na kuchochea uzeekaji wa haraka. Isije ikafikiriwa kuwa upungufu wa zinc upo zaidi kwa watu wenye lishe duni au wale katika nchi zinaendelea tu. Ukweli ni kuwa tatizo hili lipo Marekani na Ulaya kwa wanaume, wanawake na watoto.
Upungufu wa zinc hubadili namna ya kusikia ladha na kusababisha kupenda chumvi zaidi, chakula kitamu zaidi. Inaweza kujidhihirisha kwa kuharisha, upungufu wa nguvu za mwili, uchovu sugu, ugumba, upungufu wa kinga za mwili, kukosa kumbukumbu, kushindwa kutuliza mawazo, kuchelewa kupona vidonda, neva kutofanya kazi vizuri, na kuunguruma kwa sauti kwenye masikio.
Afya Ya Uzazi Ya Mwanamme:
Zinc ni madini ya lazima katika kuweka testosterone kwenye kiwango kinachotakiwa, na seli za tezi dume ya mwanamme zinahitaji kiwango cha zinc ambacho ni mara 10 zaidi ya mahitaji ya seli nyingine za mwili ili ziwe na afya na zifanye kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Upungufu wa zinc kwa wanaume huathiri uzalishaji wa testosterone, huwaweka wanaume kwenye mazingira hatarishi ya kupata saratani ya tezi dume, na huwasababishia ugumba. Upungufu wa zinc umehusishwa na kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Afya Ya Uzazi Ya Mwanamke:
Kwa wanawake, zinc inahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.
FAIDA ZINGINE ZA YA MADINI YA ZINC NI
Kuboresha Kinga Za Mwili:
Upungufu wa Zinc unaathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa kinga za mwili kwa sababu upungufu huo husababisha kudorora kwa haraka kwa ufanyaji kazi wa T cell. T cells huinua kinga za mwili wakati virusi, bakteria , au changamoto nyingine zinapotokea. watu wenye umri mkubwa huwa kwenye hatari ya kuwa na upungufu, sababu kubwa ikiwa ni kukosa zinc ya kutosha kutoka kwenye milo yao. Kuna ushahidi wa kuonyesha kuwa mahitaji ya zinc huongezeka na umri ili kuzuia uvimbe, kusaidia kinga za mwili , na kuhakikisha ufanyaji kazi wa seli unaotakiwa.
Kulinda Mfumo Wa Mishipa Ya Moyo:
Zinc ni muhimu katika kuweka sawa afya ya seli za mishipa ya moyo na endothelium. Endothelium ni tabaka jembamba la seli zinazotanda juu ya mishipa ya damu na zina mchango mkubwa katika mzunguko wa damu. Kiwango kidogo cha zinc kinaweza kusababisha kuzuiwa kwa endothelium na kusababisha kuongezeka kwa cholesterol na uvimbe. Cholesterol na uvimbe huongeza uwezekano wa kutokea magonjwa ya moyo.
Zinc huhitajika katika kuhakikisha homoni nyingi zinafanya kazi vizuri, pamoja na insulin. Zinc hunata kwenye insulin na kusababisha insulin kuhifadhiwa kwa wingi ndani ya kongosho na kutolewa pale glucose inapoingia kwenye mfumo wa damu. Pili, zinc inaisaidia insulin kunata kwenye seli na kufungua mlango ili glucose iweze kuingia. Ikiwa seli hazitataka kuipokea insulin, glucose itabakia ndani ya mfumo wa damu, itasababisha kiwango cha sukari kuwa juu, na kusababisha kuongezeka kwa mafuta. Kiwango cha zinc kinaposhuka, utolewaji wa insulin utapungua na pia upokewaji wa insulin hiyo, ambapo hali ikiendelea, tatizo la kisukari hutokea. Utafiti wa hivi karibuni huko Hispania uliohusisha wanafunzi ulionyesha uhusiano wa moja kwa moja kati ya upungufu wa zinc, uwingi wa mafuta mwilini, na mwili kutoipokea insulin.
Antioxidant Yenye Nguvu
Zinc ni antioxidant bora inayoondoa radikali huru zinazoharibu seli za mwili kwa kuungana nazo na kisha kupoteza chaji zao. Zinc hulenga radikali huru ambazo husababisha uvimbe mwilini na hasa inafanya kazi vizuri sana kuondoa sumu za metali nzito kutoka katika ubongo.
Kiondoa Sumu Chenye Nguvu
Kudorora kwa afya ya neva na ugonjwa wa Alzheimer's huchochewa na kujikusanya kwa metal nzito katika ubongo. Zinc husaidia kuondoa sumu hizi na kusaidia katika kuboresha ufanyaji kazi wa seli za ubongo (cellular homeostasis). Zinc ina mchango mkubwa sana katika shughuli za mawasiliano baina ya neva na husaidia kuweka sawa afya na umbo la ubongo. Pia, zinc ni sehemu ya kimeng'enya kinachohusika katika kuvunjavunja mafuta katika ngozi nyembamba inayofunika ubongo. Hii ni kazi muhimu sana kwa sababu katika kutunza afya ya ubongo na ufanyaji wake kazi, inatakiwa kuhakikisha kuwa ngozi hii nyembamba inapata virutubisho inavyovihitaji.
Kuzuia Kansa
Kuweka viwango vizuri vya zinc katika miili yetu kumeonyesha kuwa kunaweza kusaidia kuponya matatizo mengi sugu ya kiafya, hasa kansa na upungufu wa kinga za mwili. Pamoja na kansa ya tezi dume, upungufu wa zinc umeonyesha kuhusika sana katika kujenga karibu aina zote za kansa. Utafiti wa hivi karibuni umehusisha upungufu wa zinc na kansa za maziwa, utumbo mkubwa, ovari, mapafu , ngozi, na leukemia.
NB, kama una matatizo ya ugumba na kutopata motto basi nashauri mke na mume wafike kituo cha afya wote wawili waweze kupata vipimo ili kujua chanbzo cha tatizo hapo ndipo wanaweza kuanza kutumia dawa.
Comments
Post a Comment