Posts

Image
Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni. Zifuatazo ni baadhi tiba ambazo ni rahisi kuandaa mwenyewe ukiwa nyumbani na hazina madhara kabisa kiafya. 1. CHAI YA KIJANI (GREEN TEA) Green tea ni tajiri wa polyphenol,ina antioxidant yenye nguvu sana ambayo itaondoa plaque kuenea kwenye meno yako. Polyphenols imeonekana kuzuia bacteria kukua katika mdomo.Kwahiyo kufyonza chai ya kijani husaidia kuondoa harufu chafu ya vitunguu. Spinach, chai ya rangi,apples na mushrooms pia nazo zina polyphenols, unaweza pia kutumia aina hii ya vyakula na kinywaji baada ya kujiona mdomo unatoa harufu iliosababishwa na mlo wako. 2. MATUNDA NA MBOGA FRESH Fiber-nyingi hupatikana kwenye matunda na mboga, husaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomoni (na ku...

KIPATO CHA ZIADA

* FOREVER BUSINESS BUILDERS * 👉 * MILIKI BIASHARA YAKO LEO * Hello! Habari yako ndugu! Naitwa * Emmanuel Mputa * ,ni mwajiliwa binafsi na Mjasiriamali pia. 👉Leo napenda kukushirikisha Wazo kubwa  la biashara na Kipato, ambalo mimi Kwasababu nilikuwa na nia ya kutimiza Malengo yangu niliweza kulifanyia kazi na mpaka sasa nimetimiza malengo yangu mengi kwa kupitia fursa hii pekee. * INAWEZA KUWA NI WEWE AU RAFIKI YAKO * 👉Je unafahamu watu wengi kwa sasa wanatafuta njia mbalimbali za kuweza kujiongezea njia nyingine za vipato ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku? Hii ni  kutokana na gharama za maisha kupanda sana? Hali hii hufanya wengi wanakuwa bize sana na baadhi hujikuta wakianzisha vitu mbalimbali Lakini kutokana na kutokuwa na ufahamu au ujuzi huo, hujikuta vikifa mapema na kuwaachia hasara pasipo kuingiza faida yoyote. Lakini pia baadhi ya watu hujikuta wakiingia katika Minyororo mizito ya Madeni na Mikopo ili kuweza kukidhi mahitaji yao....

Glory na mauamivu

Nimemsikiliza Glory...  Nimemsikiliza zaidi ya mara moja...  Najaribu kulitazama hili jambo kiundani zaidi, tunachokiona kwa Glory ni matokeo ya jambo fulani na sio chanzo cha jambo hilo! Huwezi kutatua tatizo kwa kushughulika na matokeo bali jambo hutatuliwa kwa kushughulika na chanzo! Chanzo cha haya yanayompata Glory ni nini? Kwanini yupo hivi? Tatizo ni yeye au ni wanaume anaokutana nao? Glory ni mtu wa aina gani? Ana marafiki wa aina gani? Amelelewa  katika familia ya namna gani? Malezi yake yapo vipi? Alianza mapenzi katika umri gani? Je amewahi kuumizwa? Mapenzi kwake yanamaanisha nini,? Tukiweza kujibu nusu ya haya maswali tutapata mwanga kuhusu chanzo cha matatizo ya Glory. Kumwambia tu ajitahidi sio msaada anaouhitaji, Glory amekwama, anahitaji nuru na ukiona mtu anasema shida yake hadharani ujue imefika katika viwango vya juu....  Hakuna mtu anayependa kuyasema matatizo yake ila yakizidi vinywa hufunguka vyenyewe! Shida ya Glory ipo katika makuzi yake ni t...

Group O Immunity

Inasemekana watu wenye damu ya group O immunity yao ni kali kiasi cha kwamba inasababisha uwezekano wa kupata mtoto uwe mdogo. Hata magonjwa madogo madogo huwa ya malizwa kiaina. Ninachojua mtu mwenye blood group O ana antibodies 'a' na 'b' kwa sababu hana antigen. Hizi antibodies ni muhimu sana kwa ulinzi wa mwili yaani zinafanya response faster sana inapotokea kitu kigeni kimeingia katika blood serum, kitu hicho kigeni ndo kinaitwa antigen. Makundi mengine kama  Blood group A wana antigen A na antibody 'b' Blood group B wana antigen B na antibody 'a' Kwa wenye group O wanakua hawana antigen yoyote hivyo wanakua na antibodies za aina zote yaan a na b. Ambazo hizi zinaleta ulinzi mkubwa sana kwa watu hawa wenye blood group O. Watu wenye blood A na B wao wana ulinzi wa kawaida kwa sababu wana antibody moja moja either mtu anakua na 'a' au 'b' Na ningependa kufahamu pia endapo wazazi mmoja atakua na kundi la A+ ama B+ na mwingine akawa na O...

SABABU ZINAZOSABABISHA WANAWAKE KUKOSA HEDHI

Image
Hizi ni sababu zinazosababisha Wanawake Kukosa Hedhi Ni Dhahiri kuwa kukosa au kutopata kabisa hedhi ni tatizo linalowapata wanawake wengi. Kwanza kabisa ni vyema mwanamke akatambua ukweli kuwa, kukosa hedhi ni tatizo la kiafya, hata kama lisipoambatana na maumivu yoyote lakini mwanamke anapaswa kulitilia umakini wa hali ya juu. Kwa sababu, kibaiolojia hedhi ya kila mwezi inatokana na mfumo unaojiendesha wenyewe ndani ya mwili pasipo ridhaa ya mwanamke husika, hivyo kutopata hedhi kunaashiria kuwa kuna tatizo kwenye moja ya mifumo aidha wa homoni au wa uzazi na kusababishwa na matatizo mengine. Tatizo hili kwa kitaalam linaitwa amenorrhea, ni kukosekana kwa mzunguko mmoja au zaidi ya hedhi. Kwa mwanamke aliyekosa hedhi kwa miezi mitatu mfululizo na kwa wasichana walio na umri zaidi ya miaka ya wastani wa 15-18 ambao hawajapata hedhi kwa pamoja, wapo kwenye kundi hili. Sababu kuu ya kukosa hedhi ambao wengi pia tumeizoea ni ujauzito. Kwa kawaida mwanamke hapati hedhi kwa kipindi chote c...

Kunenepa Kupita Kiasi Husababishwa na Nini?

“Tunakabili tatizo kubwa ambalo linaweza kuathiri sana afya ya watoto wetu. Hatua isipochukuliwa sasa ili kuzuia tatizo hilo, watu watazidi kunenepa kupita kiasi.”—William J. Klish, profesa wa magonjwa ya watoto. WATU fulani wasio na tatizo la kunenepa huwachambua watu walionenepa kupita kiasi na kuwaona kuwa wavivu na goigoi. Lakini je, kweli tatizo hilo ni dogo hivyo? Je, kunenepa kupita kiasi ni tatizo la watu wavivu wasiopenda kufanya mazoezi? Au je, mara nyingi tatizo hilo husababishwa na mambo makubwa ambayo ni vigumu kuyazuia? Je, Husababishwa na Urithi, Mazingira, au Yote Mawili? Kitabu  Food Fight  kinasema hivi: “Kwa muda mrefu watu wamejadili ikiwa kunenepa kupita kiasi husababishwa na urithi au mazingira.” Ni nini maana ya urithi katika habari hii? Wengine husema kwamba kwa kawaida mwili wa mwanadamu huhifadhi kalori za ziada kwa ajili ya mahitaji ya wakati ujao. Kitabu hicho kinaendelea kusema: “Kwa makumi ya miaka, uchunguzi umefanywa ili kugundua jinsi urit...

Magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu.

Image
Niliwahi soma habari moja iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania ikimkariri Dk. Ali Mzige akisema ‘afya za watanzani hatarini’. Nilishawishika kuisoma habari yote kwani alichokisema ndiyo hali halisi ambayo inahitaji kutiliwa msisitizo ili watu waelimike na wajue jinsi ya kujiepusha na hatari hiyo. Dk. Mzige, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya IMTU na Mtaalamu wa Afya ya Jamii , alisema kuwa magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu yanaongezeka nchini kwa kasi na inakadiriwa ifikapo mwaka 2020, magonjwa hayo yatachukua zaidi ya ailimia 70 ya magonjwa yote. Aidha, katika habari hiyo, Dk. Mzige alisema kuwa magonjwa hayo hujulikana pia kama ‘magonjwa ya kusendeka’ (chronic disease) ambayo hutokana na ulaji mwingi wa vyakula vya kusindika (processed food) na kuacha kula vyakula vya asili. Kwa kawaida, vyakula hivyo vya kusindika, au vya kwenye makopo kama vinavyojulikana, mara nyingi huwa na mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi, kemikali nyingi na viungo ba...