Group O Immunity

Inasemekana watu wenye damu ya group O immunity yao ni kali kiasi cha kwamba inasababisha uwezekano wa kupata mtoto uwe mdogo. Hata magonjwa madogo madogo huwa ya malizwa kiaina.

Ninachojua mtu mwenye blood group O ana antibodies 'a' na 'b' kwa sababu hana antigen. Hizi antibodies ni muhimu sana kwa ulinzi wa mwili yaani zinafanya response faster sana inapotokea kitu kigeni kimeingia katika blood serum, kitu hicho kigeni ndo kinaitwa antigen.

Makundi mengine kama 
Blood group A wana antigen A na antibody 'b'

Blood group B wana antigen B na antibody 'a'

Kwa wenye group O wanakua hawana antigen yoyote hivyo wanakua na antibodies za aina zote yaan a na b. Ambazo hizi zinaleta ulinzi mkubwa sana kwa watu hawa wenye blood group O.

Watu wenye blood A na B wao wana ulinzi wa kawaida kwa sababu wana antibody moja moja either mtu anakua na 'a' au 'b'



Na ningependa kufahamu pia endapo wazazi mmoja atakua na kundi la A+ ama B+ na mwingine akawa na O watoto watakaozaliwa makundi yao ya damu inawezekana wakawa na makundi yapi? Na je kuna madhara yeyote kiafya kwa watoto watakao zaliwa?
Hizo alama za kujumlisha zinamaanisha uwepo wa 'Rhesus factor' hii ni aina flani ya protein inayoweza kuwepo kwenye damu. Kwa wasio nayo tunawaita - yaani negative kwa maana kwamba hawana hiyo protein.

Mtu mwenye damu group A kuna probability mbili inaweza kua ni damu group AA yaani Homozygous au ikawa ni AO yaani heterozygous, ila wote wataitwa kua wana damu group A.

Na mtu mwenye damu group B anaweza kua ni dam group BB ikimaanisha homozygous au BO ikimaanisha heterozygous.

Probability ya kupata watoto inategemea ni damu group gani tutatumia. Tazama hapa chini.

Suppose Mzazi ana damu group AA na mwenzie ana damu group OO.
Watoto wao wote watakua na damu group AO yaani damu group A. 

Pia anaweza kua mzazi huyo wa mwanzo ana damu group AO na mwenzie ana damu group OO kama kawaida, watoto watakua na damu group AO yaani damu group A, au damu group OO.

Tuhamie damu group B, hapa mchanganuo ni ule ule kama kwenye Damu group A tulivyofanya.
Suppose ni damu group BB na mzazi mwingine ni dam group OO, watoto wote watakua damu group BO yaani wote ni dam group B.

Kama mzazi atakua ni dam group BO na mwenzie ni dam group OO basi watoto watakua BO au OO.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

Madini ya Zink na Ugumba