Posts

Glory na mauamivu

Nimemsikiliza Glory...  Nimemsikiliza zaidi ya mara moja...  Najaribu kulitazama hili jambo kiundani zaidi, tunachokiona kwa Glory ni matokeo ya jambo fulani na sio chanzo cha jambo hilo! Huwezi kutatua tatizo kwa kushughulika na matokeo bali jambo hutatuliwa kwa kushughulika na chanzo! Chanzo cha haya yanayompata Glory ni nini? Kwanini yupo hivi? Tatizo ni yeye au ni wanaume anaokutana nao? Glory ni mtu wa aina gani? Ana marafiki wa aina gani? Amelelewa  katika familia ya namna gani? Malezi yake yapo vipi? Alianza mapenzi katika umri gani? Je amewahi kuumizwa? Mapenzi kwake yanamaanisha nini,? Tukiweza kujibu nusu ya haya maswali tutapata mwanga kuhusu chanzo cha matatizo ya Glory. Kumwambia tu ajitahidi sio msaada anaouhitaji, Glory amekwama, anahitaji nuru na ukiona mtu anasema shida yake hadharani ujue imefika katika viwango vya juu....  Hakuna mtu anayependa kuyasema matatizo yake ila yakizidi vinywa hufunguka vyenyewe! Shida ya Glory ipo katika makuzi yake ni t...

Group O Immunity

Inasemekana watu wenye damu ya group O immunity yao ni kali kiasi cha kwamba inasababisha uwezekano wa kupata mtoto uwe mdogo. Hata magonjwa madogo madogo huwa ya malizwa kiaina. Ninachojua mtu mwenye blood group O ana antibodies 'a' na 'b' kwa sababu hana antigen. Hizi antibodies ni muhimu sana kwa ulinzi wa mwili yaani zinafanya response faster sana inapotokea kitu kigeni kimeingia katika blood serum, kitu hicho kigeni ndo kinaitwa antigen. Makundi mengine kama  Blood group A wana antigen A na antibody 'b' Blood group B wana antigen B na antibody 'a' Kwa wenye group O wanakua hawana antigen yoyote hivyo wanakua na antibodies za aina zote yaan a na b. Ambazo hizi zinaleta ulinzi mkubwa sana kwa watu hawa wenye blood group O. Watu wenye blood A na B wao wana ulinzi wa kawaida kwa sababu wana antibody moja moja either mtu anakua na 'a' au 'b' Na ningependa kufahamu pia endapo wazazi mmoja atakua na kundi la A+ ama B+ na mwingine akawa na O...

SABABU ZINAZOSABABISHA WANAWAKE KUKOSA HEDHI

Image
Hizi ni sababu zinazosababisha Wanawake Kukosa Hedhi Ni Dhahiri kuwa kukosa au kutopata kabisa hedhi ni tatizo linalowapata wanawake wengi. Kwanza kabisa ni vyema mwanamke akatambua ukweli kuwa, kukosa hedhi ni tatizo la kiafya, hata kama lisipoambatana na maumivu yoyote lakini mwanamke anapaswa kulitilia umakini wa hali ya juu. Kwa sababu, kibaiolojia hedhi ya kila mwezi inatokana na mfumo unaojiendesha wenyewe ndani ya mwili pasipo ridhaa ya mwanamke husika, hivyo kutopata hedhi kunaashiria kuwa kuna tatizo kwenye moja ya mifumo aidha wa homoni au wa uzazi na kusababishwa na matatizo mengine. Tatizo hili kwa kitaalam linaitwa amenorrhea, ni kukosekana kwa mzunguko mmoja au zaidi ya hedhi. Kwa mwanamke aliyekosa hedhi kwa miezi mitatu mfululizo na kwa wasichana walio na umri zaidi ya miaka ya wastani wa 15-18 ambao hawajapata hedhi kwa pamoja, wapo kwenye kundi hili. Sababu kuu ya kukosa hedhi ambao wengi pia tumeizoea ni ujauzito. Kwa kawaida mwanamke hapati hedhi kwa kipindi chote c...

Kunenepa Kupita Kiasi Husababishwa na Nini?

“Tunakabili tatizo kubwa ambalo linaweza kuathiri sana afya ya watoto wetu. Hatua isipochukuliwa sasa ili kuzuia tatizo hilo, watu watazidi kunenepa kupita kiasi.”—William J. Klish, profesa wa magonjwa ya watoto. WATU fulani wasio na tatizo la kunenepa huwachambua watu walionenepa kupita kiasi na kuwaona kuwa wavivu na goigoi. Lakini je, kweli tatizo hilo ni dogo hivyo? Je, kunenepa kupita kiasi ni tatizo la watu wavivu wasiopenda kufanya mazoezi? Au je, mara nyingi tatizo hilo husababishwa na mambo makubwa ambayo ni vigumu kuyazuia? Je, Husababishwa na Urithi, Mazingira, au Yote Mawili? Kitabu  Food Fight  kinasema hivi: “Kwa muda mrefu watu wamejadili ikiwa kunenepa kupita kiasi husababishwa na urithi au mazingira.” Ni nini maana ya urithi katika habari hii? Wengine husema kwamba kwa kawaida mwili wa mwanadamu huhifadhi kalori za ziada kwa ajili ya mahitaji ya wakati ujao. Kitabu hicho kinaendelea kusema: “Kwa makumi ya miaka, uchunguzi umefanywa ili kugundua jinsi urit...

Magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu.

Image
Niliwahi soma habari moja iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania ikimkariri Dk. Ali Mzige akisema ‘afya za watanzani hatarini’. Nilishawishika kuisoma habari yote kwani alichokisema ndiyo hali halisi ambayo inahitaji kutiliwa msisitizo ili watu waelimike na wajue jinsi ya kujiepusha na hatari hiyo. Dk. Mzige, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya IMTU na Mtaalamu wa Afya ya Jamii , alisema kuwa magonjwa yatokanayo na tabia za binadamu yanaongezeka nchini kwa kasi na inakadiriwa ifikapo mwaka 2020, magonjwa hayo yatachukua zaidi ya ailimia 70 ya magonjwa yote. Aidha, katika habari hiyo, Dk. Mzige alisema kuwa magonjwa hayo hujulikana pia kama ‘magonjwa ya kusendeka’ (chronic disease) ambayo hutokana na ulaji mwingi wa vyakula vya kusindika (processed food) na kuacha kula vyakula vya asili. Kwa kawaida, vyakula hivyo vya kusindika, au vya kwenye makopo kama vinavyojulikana, mara nyingi huwa na mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi, kemikali nyingi na viungo ba...

Athari za unene

Athari za unene uliopindukia ni kusababisha matatizo mengi ya kiafya. Kwa mtu mwenye tatizo la unene uliopitiliza huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa hatarishi kama hataweza kudhibiti tatizo kwa haraka. Madhara ya unene kupita kiasi huweza kuwa ni yale yanayoonekana  siku kwa siku au kupata magonjwa hatarishi. Matatizo ya siku kwa siku ya unene kupita kiasi: -Kupumua kwa shida -Kutokwa jasho kwingi -Kukoroma ukiwa umelala -Kushindwa kufanya shughuli za nguvu -Kujisikia mchovu mara kwa mara -Maumivu ya joint na mgongo -Kushindwa kujiamini na kutojikubali -Kujihisi umetengwa -Huweza pia kusababisha mfadhaiko Magonjwahatarishi yanayoweza kusababishwa na kuwa na unene uliopitiliza ni kama yafuatayo: - Kisukari aina ya 2 - High blood pressure - High cholestrol (lehemu nyingi) -Asthma - Kiharusi (Stroke) -Ugonjwa wa mishipa ya moyo (Coronary heart disease) -Aina tofauti za kansa kama vile kansa ya utumbo mpana,kansa ya matiti na kansa ya mfuko wa mimba - Mawe kwenye mfuko wa nyon...

Nguvu za kiume

Image
  Jua tatizo la nguvu za kiume Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote. Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME SIYO UGONJWA, ni DALILI YA UGONJWA. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake.  Kuna sababu zaidi ya 200 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume. Mtu aweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo?  Nguvu za kiume ni nini? Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo lenyewe.  Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume? Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50n...