Posts

UTUMBO KUZIBA

Image
Utumbo kuziba Iwapo kuna kitu ambacho kimeziba sehemu yoyote ile ya utumbo, chakula na kinyesi haviwezi kupita. Hii inaweza kusababisha maumivu na maambukizi. Pamoja na maumivu, mtu huyu anaweza kuanza kupata choo kigumu au kutopata choo kabisa na kutapika. Tumbo linaweza kuwa kimya, au kutoa sauti nyingi zenye mlio wa juu. Uzibe utumboni huweza kusababisha kutapika kwa nguvu. Tatizo la utumbo kuziba linaweza kusababishwa na: Fungu la minyoo lililojisokota kama mpira . Henia . Sehemu ya tumbo kujisokota kutokana na kovu la zamani. Hii inaweza kumtokea mtu ambaye aliwahi kupata jeraha au kufanyiwa upasuaji kwenye utumbo. Saratani . Kama unadhani kuna uzibe kwenye utumbo, fanya mambo 2: Mpeleke mgonjwa hospitali mara moja.  Huenda upasuaji ukahitajika. Kama kuna minyoo mahali unapoishi, mpe dawa ya minyoo ya askarisi ukiwa unampeleka hospitalini, hasa kama minyoo ndiyo itakuwa imesababisha uzibe huo. Bonyeza hapa kwa ajili ya  dawa za minyoo . Ugonjwa wa kidole tumbo na uvi...

Maumivu tumboni au kwenye utumbo

Image
Maumivu tumboni au kwenye utumbo Kama kuna maumivu, muulize mgonjwa aoneshe hasa wapi maumivu yalipo. Mahali maumivu yalipo inaweza kutoa mwanga juu ya kisababishi. Pia ni muhimu kujua kama matumbo yanafanya kazi – kutembeza chakula na kukichakata. Kama hapana, hii inaweza kuwa dalili ya hatari hasa. Uliza:  mgonjwa amekwenda haja kubwa au kujamba? Kama anapata choo kama kawaida ni dalili nzuri. Kama mgonjwa hajaenda chooni kwa siku kadhaa, anaweza kuwa na tatizo la  kupata choo kigumu . Kama hajapata choo, hawezi kujamba, na ana maumivu, tatizo linaweza kuwa  uzibe kwenye utumbo . Sikiliza:  kuna sauti zozote kutoka kwenye utumbo? Sauti ni dalili nzuri kiafya za chakula kuchakatwa na utasikia sauti hata kama kuna tatizo la ugumu wa choo. Kutokuwa na sauti ni dalili hatari ya utumbo kuziba. Gusa:  je tumbo ni gumu kama ubao? Unapogusa anasikia maumivu sana? Hizi ni dalili za hatari kubwa. Kidonda tumboni Maumivu sehemu ya katikati tumboni Kidole tumbo Kwanza ...

TRA ruksa kutembea na polisi ukusanyaji kodi

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameibariki Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwatumia TAKUKURU pamoja na Jeshi la Polisi wenye silaha za moto wakati wanapokwenda kukusanya mapato pamoja na kodi kwa wafanyabiashara ambao ni wanaodaiwa sugu. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni Mjini Dodoma, amesema ni sahihi kwa kikosi kazi hicho (task force) kutumika kwa kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara sugu wenye lengo baya la kutotaka kulipa madeni na badala yake hutoa rushwa. Mhe. Lema alitaka kusikia kauli ya serikali juu ya mfumo unaotumiwa TRA wa kusumbua na kuwatisha wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku huku ikiwa inadaiwa kuwa mamlaka hiyo hutumia Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza , Arusha na Mbeya. “Ni kweli kwamba tunacho chombo ambacho kinachowajibika katika ukusanyaji wa mapato na kodi kutoka kwa...

KUIMARISHA NGOZI YAKO

Image
Wote tunapenda kuonekana warembo na vijana. Lakini inawezekana ukawa unajiharibu zaidi katika kujifanya uwe mrembo leo na kujiletea madhara makubwa yasiyotibika kesho. Pia, inawezekana unatumia hela nyingi na muda mwingi katika kuhakikisha ngozi yako inakuwa nyororo, nzuri, na ya kuvutia. Je, unafahamu kuwa kuna aina za vyakula vinavyosaidia katika kutunza ngozi yako? Kama ambavyo unajitahidi kufuata kanuni za afya ili kuufanya mwili wako uwe vizuri – chakula bora, mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu – vivyo hivyo ngozi yako inatakiwa kutunzwa kutokana na kanuni asilia. Hapa tunakuletea vyakula vinavyotunza ngozi yako bila gharama yeyote. 1. Asali Asali ni afya kwa binadamu, hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia. Chochote kile ambacho ni kizuri kwa afya yako ni nzuri kwa ngozi pia. Ngozi yenye afya inatakiwa kuhifadhi unyevunyevu ili kuzuia kukauka na kupasuka. Hii ndio sababu kubwa ya kutumia mafuta ili kuweka ngozi iwe na unyevunyevu. Asali husaidia kuleta na kuhifadh...

FIVE WAYS TO IMPROVE YOUR REPRODUCTIVE HEALTH THROUGH DIET [FOR MEN AND WOMEN ]

Image
CUT OUT ALCOHOL Alcohol isn't just bad during pregnancy, but it can also reduce fertility in both men and women. Alcohol can have a negative impact on sperm quality and testosterone levels, and can also reduce your overall sperm count. Alcohol is also suspected to reduce fertility in women and scientists suspect alcohol consumption is one of the reasons behind an increase in infertility in women. Although it's not necessary to completely stop drinking, try to take in no more than one to two drinks a day. If you've gone many months without conceiving, try ceasing your alcohol intake entirely, and see if this step doesn't help you conceive. EAT PLENTY OF FRUITS AND VEGETABLES Fruits and vegetables such as arugula, kale, blueberries, oranges, red peppers and raspberries are full of vitamins, antioxidants and phytonutrients. These properties can help feed and repair your reproductive system. Furthermore, environmental factors such as smog, pollution and stressors can contri...

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The Essentials Of Business Etiquette

Image
Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wangu? ni matumaini yangu kuwa umeamka salama siku hii ya leo. Leo ni siku nyingine bora sana na ya kipekee kwetu hivyo tunaalikwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo. Rafiki, tumia muda wako vema kwa manufaa yako mwenyewe na dunia nzima. Karibu sana rafiki katika makala yetu ya leo ambapo leo nitakwenda kukushirikisha mambo muhimu niliyojifunza katika uchambuzi wa kitabu. Nitakwenda kukushirikisha mambo machache kati ya mengi kupitia kitabu hiki. Karibu tuanze pamoja hadi tamati ya somo letu la leo. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Barbara Pachter. Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha The Essentials of Business etiquette na Barbara Pachter ni kama ifuatavyo; 1. Jina ni muhimu sana. Kila mtu ana jina lake na amepewa jina ili atambulike yeye ni nani. Jina linatambulisha biashara ya mtu. Jina linabeba biashara au kitu unachofanya. Kama unamwita mtu jina lake mwite kiufasaha na siyo jina la utani. Mara nyingi pen...

Njia 14 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni

Image
Kati ya matatizo makubwa kabisa yanayowasumbuwa wanaume katika suala la kujamiiana ni  kufika kileleni mapema . Takwimu zisizo rasmi zinasema kuwa, wanaume 7 kati ya 10 wanapatwa na tatizo hii. Malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wanaume yanathibitisha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika mbili kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu wakati wakiandaana na kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa. Hata hivyo wale wanaoweza kusimama tena mara baada ya tendo la kwanza wanakiri kuchelewa kidogo, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi wa rika zote vijana hata wazee. Ndoa nyingi zimevunjika chanzo kikiwa ni tatizo hili. Karibu kila pembe ya dunia kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni, ambalo limewafanya waonekane si lolote kwa wenzi wao. Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya ...