KUIMARISHA NGOZI YAKO
Wote tunapenda kuonekana warembo na vijana. Lakini inawezekana ukawa unajiharibu zaidi katika kujifanya uwe mrembo leo na kujiletea madhara makubwa yasiyotibika kesho. Pia, inawezekana unatumia hela nyingi na muda mwingi katika kuhakikisha ngozi yako inakuwa nyororo, nzuri, na ya kuvutia. Je, unafahamu kuwa kuna aina za vyakula vinavyosaidia katika kutunza ngozi yako?
Kama ambavyo unajitahidi kufuata kanuni za afya ili kuufanya mwili wako uwe vizuri – chakula bora, mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu – vivyo hivyo ngozi yako inatakiwa kutunzwa kutokana na kanuni asilia. Hapa tunakuletea vyakula vinavyotunza ngozi yako bila gharama yeyote.
1. Asali
Asali ni afya kwa binadamu, hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia. Chochote kile ambacho ni kizuri kwa afya yako ni nzuri kwa ngozi pia. Ngozi yenye afya inatakiwa kuhifadhi unyevunyevu ili kuzuia kukauka na kupasuka. Hii ndio sababu kubwa ya kutumia mafuta ili kuweka ngozi iwe na unyevunyevu. Asali husaidia kuleta na kuhifadhi unyevunyevu kwenye ngozi.
Ili kuweza kulinda ngozi, paka asali wakati wa kuoga, acha kwa muda kisha ioshe. Ni zoezi la muda mfupi linalohakikisha ngozi yako inanawiri vizuri.
Asali ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambavyo huzuia vijidudu (Bacteria) wanaozaliana kwenye ngozi.
2. Vyakula vya baharini
Kwa ujumla vyakula vya baharini ni vizuri kwa afya yako, lakini faida haishii kwenye afya ya mwili tu, bali inasaidia hata kwenye ngozi yako. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega-3 ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi yako.
Faida za Omega3
Kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi.Kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi.Husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi - mzunguko mzuri wa damu mwilini ni muhimu kwa ngozi yenye afya.
Faida za Zinc kwa ngozi
Inasaidia kuondoa chunusi na harara kwa kuyeyusha homoni ya testosterone.Inasaidia kuzalishwa kwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa. Hii inaifanya ngozi kung’aa na kuwa na mvuto.
3. Mayai
Nadhani si ajabu kusema kuwa yai ni kirutubisho muhimu kwa afya yako. Lakini afya yako huonekana kutokana na ubora wa ngozi yako. Yai lina virutubisho muhimu sana – iwe kiingi au ute – kwa afya ya ngozi yako. Kiini cha yai kina vitamin A, na B. Ute wa yai una protini nyingi ambayo ni muhimu pia kwa ngozi yako.
Tretinoin inayopatikana kwenye Vitamin A kwa ngozi yako ni kuwa inasaidia kuondoa chunusi na mikunjo ya ngozi.Biotin inayopatikana kwenye Vitamin B ni muhimu kwa afya ya ngozi na kucha.Protini inayopatikana kwenye ute wa yai ni muhimu kufanya ngozi kuwa nyororo na yenye kung’aa na kusaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.
4. Matunda
Matunda yenye vitamin C – chungwa, limao na mengine mengi – ni muhimu kwa afya ya ngozi yako sababu inasaida kutengeneza collagen, aina ya protini inayotengeneza ngozi.
Vitamin C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi hivyo kuilinda ngozi yako kuzeeka mapema.
5. Shayiri
Shayiri ina virutubisho muhimu vya kuisaidia ngozi yako. Hivi ni kama
Mafuta yanayolainisha ngoziPolysaccharides ambayo huzuia kupasuka kwa ngozi kutokana na ukavuSaponins, inayosaidia kusafisha ngozi na kuzuia fungus na vijiduduPolyphenols inayozuia uvimbe wa ngoziProtini inayojenga na kurutubisha ngoziWanga unaohifadhi unyevunyevu kwenye ngozi
6. Mboga za majani
Mboga za majani zina vitamini A nyingi sana. Vitamin A ni muhimu kwenye ngozi sababu ndio kitu kikubwa kwenye kusaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya kungara na kuvutia.
7. Shea Butter
Mafuta ya shea ni kirutubisho muhimu kinachotumika kwa muda mrefu sana katika kutibu magonjwa mengi, hasa katika nchi za Afrika. Mafuta ya shea yana triglycerides, mfanopalmitic, stearic, oleic and linoleic fatty acids. Hivi ni muhimu katika kuleta unyevunyevu na kulinda ngozi kwa muda mrefu.
8. Karanga
Vyakula jamii ya karanga vina vitamin E ambayo ni muhimu katika kuzuia kuzeeka kwa ngozi hasa kutokana na kupigwa sana na jua. Vitamin E pia husaidia ngozi kuhifadhi unyevunyevu na hivyo kuifanya ngozi kuwa inang’aa na nyororo.
9. Maziwa ya Mbuzi
Maziwa ya mbuzi yana Vitamin A, E na Lactic acid. Lactic acid husaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuacha ngozi ikiwa na seli zilizo hai, hivyo kuifanya iwe na afya.
Maziwa ya mbuzi pia yana Caprylic Acid ambayo ni muhimu kwenye kupunguza kiwango cha asid kwenye ngozi – hii inasaidia kuzuia mazalia ya bakteria na vijidudu kwenye ngozi vilevile kusaidia ngozi kufyonza virutubishi kirahisi.
10. Nafaka isiyokobolewa
Vyakula visivyokobolewa vina virutubisho vingi zaidi na vina faida kubwa zaidi kwenye afya ya mwili pamoja na ngozi yako. Mfano ngano ni chanzo muhimu cha Vitamin B – Biotin ambayo inasaidia seli kutengeza mafuta na hivyo kuzuia kupasuka na kukatika kirahisi.
Wasiliana Nami kwa...
+255767962720
mputae84@gmail.com
Comments
Post a Comment