Maumivu tumboni au kwenye utumbo
Maumivu tumboni au kwenye utumbo
Kama kuna maumivu, muulize mgonjwa aoneshe hasa wapi maumivu yalipo. Mahali maumivu yalipo inaweza kutoa mwanga juu ya kisababishi. Pia ni muhimu kujua kama matumbo yanafanya kazi – kutembeza chakula na kukichakata. Kama hapana, hii inaweza kuwa dalili ya hatari hasa.
Uliza: mgonjwa amekwenda haja kubwa au kujamba? Kama anapata choo kama kawaida ni dalili nzuri. Kama mgonjwa hajaenda chooni kwa siku kadhaa, anaweza kuwa na tatizo la kupata choo kigumu. Kama hajapata choo, hawezi kujamba, na ana maumivu, tatizo linaweza kuwa uzibe kwenye utumbo.
Sikiliza: kuna sauti zozote kutoka kwenye utumbo? Sauti ni dalili nzuri kiafya za chakula kuchakatwa na utasikia sauti hata kama kuna tatizo la ugumu wa choo. Kutokuwa na sauti ni dalili hatari ya utumbo kuziba.
Gusa: je tumbo ni gumu kama ubao? Unapogusa anasikia maumivu sana? Hizi ni dalili za hatari kubwa.
Maumivu sehemu ya katikati tumboni
Kwanza maumivu husikika hapa
Baadaye maumivu husikika hapa
Maumivu mara nyingi hufika hadi mgongoni
Maumivu hapa, wakati mwingine huenea kifuani
Maumivu mgongoni katikati au sehemu ya chini, mara nyingi yakienea kuzunguka nyonga hadi sehemu za chini tumboni.
Mimba kutunga nje ya mji wa mimba
Maumivu sehemu ya upande mmoja wa bega au shingoni
Jinsi ya kusikilizia
Sikilizia kwenye tumbo kwa kutumia kifaa maalum cha kusikilizia au sikio lako, ili kujua iwapo mgonjwa yupo hatarini. Tumbo lenye afya hutoa sauti ndogo za kugugumia kila baada ya dakika chache. (Kama wewe ni mfanyakazi wa afya, fanya zoezi la kusikilizia tumbo za watu zenye afya ili ujue sauti za kawaida zinazotolewa na tumbo hizi. Inahitaji uzoefu kuzisikia sauti hizi ndogo.)
Sauti nyingi za kugugumia zinaweza kumaanisha kuwa chakula kinatembea haraka kupita matumboni. Je mhusika ana tatizo la kuharisha?
Sauti za juu, au kutokuwa na sauti kabisa kwa dakika 2, ni dalili ya maumivu makali ya ghafla tumboni pasipo kuharisha. Jaribu kuligusa tumbo. Kama ni gumu na linauma, nenda hospitali haraka.
Jinsi ya kuhisi
Mwambie mgonjwa aguse mahali panapouma.
Ukianzia upande mkabala na mahali anapoonesha, bonyeza taratibu kuchunguza kiungo ndani ya mwili ambacho huenda ndicho chanzo cha maumivu (sehemu inayouma sana ndiyo iwe ya mwisho). Bonyeza taratibu lakini kwa mkazo, na endelea kwa mpangilio ili uweze kuchunguza kwa kugusa kila sehemu ya tumbo.
Pia angalia iwapo tumbo ni laini au gumu, na iwapo mgonjwa anaweza kuachia na kulegeza tumbo lake. Iwapo tumbo limekakamaa kama ubao, inawezekana kuna uzibe kwenye utumbo.
Jinsi ya kuchunguza maumivu ambayo hujitokeza baada ya kuondoa mkazo wa mkono kwenye tumbo
Polepole lakini kwa mkazo bonyeza tumbo, juu kidogo ya kinena, hadi litakapoanza kuuma kidogo. Halafu ondoa mkono wako haraka. Maumivu makali ya ghafla mara utakapoondoa mkono wako-makali kuliko yale ya mwanzo unapoweka mkazo wa mkono wako-yanaweza kutokea. Kama maumivu hayo hayapo upande wa kushoto, jaribu upande wa kulia. Maumivu haya ni dalili ya kidole tumbo. Nenda hospitali mara moja.
Maumivu makali tumboni yanayoibuka ghafla
Maumivu makali yanaweza kuanza ghafla, na kuendelea pasipo kuharisha. Maumivu makali tumboni pasipo kuharisha yanaweza kuashiria uzibe kwenye utumbo, kidole tumbo, mimba kutunga nje ya mji wa mimba au kizazi au matatizo mengine hatari. Kama utaona dalili hizi, unaweza kunusuru maisha ya mgonjwa kwa kumsaidia kwenda hospitali mara moja.
Dalili
Maumivu makali endelevu - kama kuchomwa au kukatwa kwa kisu kali.
Kutapika
Kupata choo mara chache au kutopata choo kabisa
Tumbo gumu, na ambalo halitoi mgugumo wowote
Kuhisi unaumwa sana
Kawaida, mgonjwa mwenye maumivu makali tumboni anakuwa anajigaragaza kutokana na maumivu, hawezi kujisikia vizuri na anakuwa akiihami tumbo lake kwa mikono yake.
+255625748804
+255767962720 whatsapp
Comments
Post a Comment