UTUMBO KUZIBA

Utumbo kuziba

Iwapo kuna kitu ambacho kimeziba sehemu yoyote ile ya utumbo, chakula na kinyesi haviwezi kupita. Hii inaweza kusababisha maumivu na maambukizi.

Pamoja na maumivu, mtu huyu anaweza kuanza kupata choo kigumu au kutopata choo kabisa na kutapika. Tumbo linaweza kuwa kimya, au kutoa sauti nyingi zenye mlio wa juu.


Uzibe utumboni huweza kusababisha kutapika kwa nguvu.

Tatizo la utumbo kuziba linaweza kusababishwa na:

Henia.

Sehemu ya tumbo kujisokota kutokana na kovu la zamani. Hii inaweza kumtokea mtu ambaye aliwahi kupata jeraha au kufanyiwa upasuaji kwenye utumbo.

Saratani.

Kama unadhani kuna uzibe kwenye utumbo, fanya mambo 2:

Mpeleke mgonjwa hospitali mara moja. Huenda upasuaji ukahitajika.

Kama kuna minyoo mahali unapoishi, mpe dawa ya minyoo ya askarisi ukiwa unampeleka hospitalini, hasa kama minyoo ndiyo itakuwa imesababisha uzibe huo. Bonyeza hapa kwa ajili ya dawa za minyoo.

Ugonjwa wa kidole tumbo na uvimbe wa ngozi ya fumbatio (peritonitis)


Maumivu yanaweza kuanzia sehemu inayozunguka kitovu

Halafu yakaendelea chini upande wa kulia.

Ugonjwa wa kidole tumbo unatokana na maambukizi ya kimfuko kidogo kilichounganika na utumbo mkubwa sehemu ya chini upande wa kulia wa tumbo. Hakuna njia ya kuzuia ugonjwa wa kidole tumbo. Hujitokeza tu kwa baadhi ya watu.

Dalili kuu ya ugonjwa wa kidole tumbo ni maumivu makali tumboni ambayo huzidi kuongezeka. Mtu mwenye ugonjwa wa kidole tumbo kawaida hapendi kula. Kawaida hakuna kuharisha. Homa ni kawaida,na mgonjwa huumia sana anapotembea au kusafiri kupita juu ya matuta ya barabarani. Ukiweka mkono sehemu hiyo na kubonyeza halafu ukaachia, maaumivu makali hutokea.

Tafuta msaada wa daktari. Kama ugonjwa huu hautatibiwa, kidole tumbo kilichoathirika kinaweza kupasuka na kusambaza vijidudu ndani ya tumbo. Hii inaweza kusababisha uambukizo hatari kwenye ngozi ya fumbatio ujulikanao kama peritonitisi.

Uvimbe wa fumbatio (Peritonitisi) unaweza pia kusababishwa na jeraha tumboni – kwa mfano kipigo kikubwa au kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni.

Kama tumbo halitoi mgugumo wowote, ni gumu na linauma lote, huenda kuna ambukizo kwenye ngozi ya fumbatio.


Kama unadhani mgonjwa ana ugonjwa wa kidole tumbo au maambukizi ya ngozi ya fumbatio(peritonitis):

Mpeleke hospitali.

Mpe dawa 2: metronidazo (metronidazole) NA sipro (ciprofloxacin) AU seftriazoni (ceftriaxone), AU ampisilini. Bonyeza hapa kwa maelekezo juu ya dozi.

Usimpe chakula chochote au kinywaji isipokuwa dawa na maji kidogo ya kumezea tu.

Chunguza kama kuna dalili za mshtuko kama vile pumzi dhaifu ya haraka haraka, rangi ya mwili kupauka, ngozi kuwa baridi; au kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu. Angalia sura ya Huduma ya kwanza.

Mimba iliyotunga nje ya mji wa mimba au kizazi



Kawaida, mimba hutunga ndani ya mji wa mimba au kizazi.

Mimba inayotunga nje ya mji wa mimba hukulia ndani ya mrija wa uzazi – lakini nafasi haitoshi. Kadri mimba inavyokua, mrija hupanuka na unaweza kupasuka. Hali hii husababisha maumivu makali na uvujaji damu ndani ya mwili.

Kama inavyokua mimba inapoharibika, dalili za mimba kutunga nje ya mji wa mimba hutokea mapema katika ujauzito — mara nyingi hata kabla mwanamke hajajua kuwa ana mimba. Kunakuwa na maumivu tumboni sehemu za chini, na uvujaji damu baada ya kutopata hedhi kwa mwezi 1 au zaidi.

Dalili

Uvujaji damu kidogo kutoka ukeni - (tofauti na uvujaji mzito wakati mimba inapoharibika).


Maumivu yanaweza kuongezeka upande mmoja.

Kama ujauzito utapasua mrija wa uzazi, maumivu huwa makali zaidi.

Mwanamke anaweza pia kuwa na maumivu begani au shingoni.

Anaweza kusikia kizunguzungu au kupepesuka kwa sababu ya kutokwa na damu nyingi.

Maumivu makali tumboni sehemu ya chini yanaweza kusababishwa na mambo mengi, yakiwemo maambukizi kwenye kibofu, kidole tumbo, na mengine. Kama inawezekana, mshauri mwanamke apimwe kujua iwapo ni mjamzito. Kama kipimo kitaonesha ndiyo, au kama huwezi kupata kipimo hicho lakini unadhani anaweza kuwa na mimba ambayo imetunga nje ya mji wa mimba, msaidie afike hospitali – unaweza kuponya maisha yake. Kama Kipimo cha mimba kitaonesha hana mimba, basi hana tatizo la mimba ambayo imetunga nje ya mji wa mimba.

Mkiwa njiani kuelekea hospitali, tibu dalili za mshtuko kama vile pumzi dhaifu inayokwenda haraka haraka; rangi ya mwili kupauka, ngozi kuwa baridi; au kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu. Angalia sura ya Huduma ya kwanza.

+255625748804

+255767962720


Comments

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

Madini ya Zink na Ugumba