Njia 14 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni
Kati ya matatizo makubwa kabisa yanayowasumbuwa wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinasema kuwa, wanaume 7 kati ya 10 wanapatwa na tatizo hii.
Malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wanaume yanathibitisha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika mbili kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu wakati wakiandaana na kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa.
Hata hivyo wale wanaoweza kusimama tena mara baada ya tendo la kwanza wanakiri kuchelewa kidogo, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi wa rika zote vijana hata wazee.
Ndoa nyingi zimevunjika chanzo kikiwa ni tatizo hili. Karibu kila pembe ya dunia kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni, ambalo limewafanya waonekane si lolote kwa wenzi wao.
Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humwacha mwanamke na huzuni kwani anakuwa hajapata kile anakihitaji katika tendo hilo.
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Njia za kujitibu tatizo la kuwahi kufika kileleni:
1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? +255672154151
2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.
Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.
Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.
4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.
Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.
5. Tumia kitunguu swaumu
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo:
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ambayo huua fangasi mbalimbali mwilini.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
kitunguu swaumu
Kigawanyishe katika punje punje
kitunguu swaumu
chukua punje 6
kitunguu swaumu
Menya punje moja baada ya nyingine
kitunguu swaumu
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
kitunguu swaumu
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!
Fanya hivi kila siku kila unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4. Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama unmepona tatizo lako.
6. Kula tikiti maji
TikitiMaji
Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.
Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.
Faida nyingine 12 za tikiti maji kiafya ukiacha hii ya nguvu za kiume
• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara.
7. Kula ugali wa dona
Ugali wa Dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.
8. Tumia chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.
9. Kunywa maji mengi kila siku
Maji ni Uhai
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.
10. Tafuna mbegu za maboga
Mbegu za maboga
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukipiga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga.
NAMNA NZURI YA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA KAMA DAWA:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga, ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kila siku. Unatafuna na ganda lake hasa kama zimekaangwa tayari
Kwa muda gani? Kwa wiki 3 mpaka 4 kwa ugonjwa wowote kati ya haya niliyoeleza. Kumbuka pia unaweza kutumia mbegu hizi hata kama huumwi chochote!
11. Tumia asali yenye mdalasini
Asali & Mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.
Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake. Unaweza kuitumia kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari. Au unaweza kuweka vijiko vikubwa vitatu ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote kutwa mara 2 amabapo husaidia pia kutibu uchovu mwilini.
12. Kunywa chai ya tangawizi
Chai ya Tangawizi
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.
Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!
13. Shiriki tendo la ndoa mara nyingi
Kuna stori zinasema twiga hakuzaliwa na shingo ndefu namna hii kama anavyoonekana akiwa mkubwa, bali wanasema ile tabia yake ya kupenda kula majani ya juu ya miti ndiyo ikapelekea shingo yake ikarefuka!. Inawezekana kuna ukweli kidogo wa stori hizi. Usinielewe vibaya wala usije ukasema huyu jamaa anahamasisha watu kufanya mapenzi! Hapana usiwe na haraka hivyo utanielewa tu ninachotaka kusema
Wanasayansi wa masuala ya mapenzi wanasema ikiwa mtu mzima hana msongo wowote wa mawazo (stress), ana afya nzuri tu ya kutosha na anakula vizuri basi anaweza kushiriki tendo la ndoa kila baada ya masaa 24. Angalia na umsome pia mwenza wako pia angalia umri wako, sababu kuna wanawake wengine kwa asili hawapendi kushiriki tendo la ndoa kila mara pia hatuwezi kusema mtu mwenye miaka 50 atakuwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kila mara kama mtu wa miaka 18 hadi 40 hivi.
Ni vigumu mtu anakaa mwenzi mzima mwingine miezi miwili mwingine anakaa miezi 6 bila kushiriki tendo la ndoa na utegemee utakuwa na uwezo wa kuchelewa kufika kileleni. Kama hushiriki tendo la ndoa kuna uwezekano mkubwa ukawa unapiga punyeto kitendo ambacho ni kibaya zaidi kwa afya ya uume wako. Kwahiyo unaweza kushiriki mara 2 hadi 3 kwa wiki na unaposhiriki tuliza akili na upate muda wa kutosha wa kuandaana kabla ya tendo na siyo haraka haraka tu (mambo ya short time).
#Mputa the king
+255672154151
+255767962720
Comments
Post a Comment