MZUNGUKO MFUPI WA HEDHI
SIKU YA UZAZI MZUNGUKO MFUPI Mungu ndio muumba watu wote na viumbe vyote juu na chini ya jua - hilo halina pingamizi wala ubishi na lazima tumshukuru Mungu kwa hilo, ila alitoa amri ya ndoa kwamba ZAENI MKAONGEZEKE kwa hiyo kila mtu anayependa kutimiza amri hii yafaa awe na maarifa. Kwa wale wasiojua namna ya kuhesabu mizunguko yao basi ni muhimu kurudi katika mada zilizopita na kisha kujifunza namna ya kuhesabu mzunguko wako. Tambua ya kwamba mzunguko wa bleed (hedhi) ni tofauti sana na siku za bleed (hedhi). 1. Siku za bleed (hedhi) ni kuanzia na siku ya kwanza unapata bleed hadi siku ile unamaliza bleed. 2. Wakati mzunguko wa bleed huanza siku umepata bleed mpaka siku moja kabla hujapata bleed nyingine. Mfano umepata bleed tarehe 1 mwezi wa saba na bleed hiyo ikaisha tarehe 05 basi siku za bleed ni 5 na zimeanza tarehe moja na zikaisha tarehe 5. Kama bleed ingine umeipta tarehe 29 mwezi wa 7. Basi mzunguko wako wa bleed ya mwezi wa saba umeanza tarehe 01 mwezi wa saba na ukaisha tar...