MZUNGUKO MFUPI WA HEDHI
SIKU YA UZAZI MZUNGUKO MFUPI
Mungu ndio muumba watu wote na viumbe vyote juu na chini ya jua - hilo halina pingamizi wala ubishi na lazima tumshukuru Mungu kwa hilo, ila alitoa amri ya ndoa kwamba ZAENI MKAONGEZEKE kwa hiyo kila mtu anayependa kutimiza amri hii yafaa awe na maarifa.
Kwa wale wasiojua namna ya kuhesabu mizunguko yao basi ni muhimu kurudi katika mada zilizopita na kisha kujifunza namna ya kuhesabu mzunguko wako. Tambua ya kwamba mzunguko wa bleed (hedhi) ni tofauti sana na siku za bleed (hedhi).
1. Siku za bleed (hedhi) ni kuanzia na siku ya kwanza unapata bleed hadi siku ile unamaliza bleed.
2. Wakati mzunguko wa bleed huanza siku umepata bleed mpaka siku moja kabla hujapata bleed nyingine.
Mfano umepata bleed tarehe 1 mwezi wa saba na bleed hiyo ikaisha tarehe 05 basi siku za bleed ni 5 na zimeanza tarehe moja na zikaisha tarehe 5.
Kama bleed ingine umeipta tarehe 29 mwezi wa 7. Basi mzunguko wako wa bleed ya mwezi wa saba umeanza tarehe 01 mwezi wa saba na ukaisha tarehe 28 mwezi wa saba. Mzunguko huo ni wa siku 28. Mzunguko wa mwezi wa 8 Umeanza tarehe 29 mwezi wa 7.
Ukiwa na mzunguko mfupi usiogope kwa kuwa bado unayonafasi kubwa ya kupata mtoto na watu wengi tu wapo wana watoto.
Lazima ujue mzunguko wako kwanza ni wa siku ngapi. Mfano kama umekuwa na mzunguko wa siku 21 kwa muda wa miezi mitatu mfululizo na mfano umepata bleed tarehe 10 mwezi wa saba basi siku yako ya uzazi haiwezi kuwa siku siku ya 14 tangu kupata bleed. Bali ni siku ya 7 tangu umepata bleed.
EBU ZAMA NDANI HAPA UJIFUNZE
Mzunguko wa siku 21 siku ya uzazi ni siku ya (7) tangu upate bleed. Kwa hiyo kama utapata bleed siku 3 basi siku ya tano unatakiwa uanze tendo la ndoa. Mfano mzuri ni kama ufuatao. >>>Marry ameingia bleed leo tarehe 16 mwezi wa 7 na mzunguko wake kila mwezi unamchukua siku 21. Huyu Marry anachukua siku 3 za bleed. Basi siku zake atahesabu hivi tarehe 16 ni siku ya kwanza yaani leo tarehe16 ni siku ya kwanza ya bleed, kesho tarehe 17 ni siku ya pili ya bleed, kesho kutwa tarehe 18 ni siku ya tatu ya bleed,tarehe 19 ni siku ya nne bleed imeisha, tarehe 20 siku ya tano bleed imeisha - anza hapa kukutano na mwenzako, tarehe 21 ni siku ya sita endelea na tendo na tarehe 22 siku ya saba endelea na tendo yai linatoka. Unashauriwa kuanza mapema ili kuongeza nafasi ya mbegu kulikuta yai.
MZUNGUKO WA SIKU 22,23,24,25 NA 26
Munguko wa siku 22 yai linatoka siku ya 8 wewe anza tendo siku ya 6, 7 na 8
Munguko wa siku 23 yai linatoka siku ya 9 wewe anza tendo siku ya 7
Munguko wa siku 24 yai linatoka siku ya 10 wewe anza tendo siku ya 8
Munguko wa siku 25 yai linatoka siku ya 11 wewe anza tendo siku ya 9
Munguko wa siku 26 yai linatoka siku ya 12 wewe anza tendo siku ya 10
Kumbuka kuanza siku moja au mbili kabla ya siku ya yai kutoka pia unaweza ongeza siku 1 au mbili baada ya siku yenyewe hi ni kwa sababu mizunguko huwa inabadilika badilika kutokana na sababu mbalimbali kama ugonjwa na dawa nzitonzitom mshituko kama wa kufiwa, kubadilika kwa hali ya hewa na pia mabadiliko ya mwili kama kunenepa.
Kumbuka kama umekaa muda mrefu hujapata mtoto ni lazima ufike hospitalini na kupima na kupata majibu sahihi. Ni muhimu pia ukawa uko karibu na mwenzako, una afya nzuri na mko vizuri kiuhusiano.
UMUHIMU WA CHAKULA BORA
Ni muhimu ule chakula bora na sio bora chakula. Imethibitika ya kwamba asilimia zaidi ya 50 ya matatizo ya hedhi hutokana na kutokula vizuri – Ulaji wa chips soda, pombe kupindukia, kula wanga mwingi na sukari ni hatari kwa maisha ya ndoa. Unatakiwa kula chakula halisi (Real Food) chakula fresh na chakula cha asili. Vyakula hatari ni pamoja na vyakula vya paketi na makopo na kuku wa kisasa (chicken)
Kwa mawasiliano
Piga +255767962720
+255625748804
Comments
Post a Comment