Athari za unene
Athari za unene uliopindukia ni kusababisha matatizo mengi ya kiafya. Kwa mtu mwenye tatizo la unene uliopitiliza huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa hatarishi kama hataweza kudhibiti tatizo kwa haraka. Madhara ya unene kupita kiasi huweza kuwa ni yale yanayoonekana siku kwa siku au kupata magonjwa hatarishi. Matatizo ya siku kwa siku ya unene kupita kiasi: -Kupumua kwa shida -Kutokwa jasho kwingi -Kukoroma ukiwa umelala -Kushindwa kufanya shughuli za nguvu -Kujisikia mchovu mara kwa mara -Maumivu ya joint na mgongo -Kushindwa kujiamini na kutojikubali -Kujihisi umetengwa -Huweza pia kusababisha mfadhaiko Magonjwahatarishi yanayoweza kusababishwa na kuwa na unene uliopitiliza ni kama yafuatayo: - Kisukari aina ya 2 - High blood pressure - High cholestrol (lehemu nyingi) -Asthma - Kiharusi (Stroke) -Ugonjwa wa mishipa ya moyo (Coronary heart disease) -Aina tofauti za kansa kama vile kansa ya utumbo mpana,kansa ya matiti na kansa ya mfuko wa mimba - Mawe kwenye mfuko wa nyon...