WAKATI NDIO HUUU
Habari ndugu msomaji wa makala zangu nimatumaini yangu kabisa uko salama tazama leo ni siku nyingine tunakutana tena ili kuhakikisha tunafuguana kifikra na mawazo unapaswa kumshukuru Mungu ambae kakupa siku hii kama zawadi Kwako na uitumie ili uweze kuongeza kitu katika maisha yako, ninaamini kabisa hata kusoma makala hii ni kuitumia Vyema siku yako maana umeongeza ufaham zaidi, moja ya kitu ambacho watu wengi hawajui kukitumia ni wakati na tena wakati ule uliopo, watu wengi sana maisha yao yanashindwa kubadilika kwasababu wanashindwa kuutumia wakati uliopo na maisha yao yamebaki kuwa yaleyale. Hayabadiliki wengine magumu bora ya jana na wengine hufa hali ya kuwa ni masikini sio kwamba hawana uwezo Bali hawako tayali kuutumia wakati hisika. Hakuna wakati mzuri wa kutengeneza mazingira ya kupata ajira kama wakati ambao uko kwenye mazoezi ya vitendo (field) najua unaweza kuniuliza kivipi hiyo ni mada ndefu endelea kufatalia makala hizi utajifunza, hakuna wakati mzuri wa kuanza kujifunza ...