WAKATI NDIO HUUU

Habari ndugu msomaji wa makala zangu nimatumaini yangu kabisa uko salama tazama leo ni siku nyingine tunakutana tena ili kuhakikisha tunafuguana kifikra na mawazo unapaswa kumshukuru Mungu ambae kakupa siku hii kama zawadi Kwako na uitumie ili uweze kuongeza kitu katika maisha yako, ninaamini kabisa hata kusoma makala hii ni kuitumia Vyema siku yako maana umeongeza ufaham zaidi, moja ya kitu ambacho watu wengi hawajui kukitumia ni wakati na tena wakati ule uliopo, watu wengi sana maisha yao yanashindwa kubadilika kwasababu wanashindwa kuutumia wakati uliopo na maisha yao yamebaki kuwa yaleyale. Hayabadiliki wengine magumu bora ya jana na wengine hufa hali ya kuwa ni masikini sio kwamba hawana uwezo Bali hawako tayali kuutumia wakati hisika.

Hakuna wakati mzuri wa kutengeneza mazingira ya kupata ajira kama wakati ambao uko kwenye mazoezi ya vitendo (field) najua unaweza kuniuliza kivipi hiyo ni mada ndefu endelea kufatalia makala hizi utajifunza, hakuna wakati mzuri wa kuanza kujifunza kuacha ajira na kujiajiri kama wakati ambao uko kwenye ajira, watu wengi wanasubiri wastaafu ndio aanze kujifunza biashara kwanini usianze sasa ili ukistaafu uwe tayali umekuwa mtaalam Anza basi hata kwa kuhudhuria mafunzo siku moja moja utaona milango inaanza kufunguka, rafiki maisha ya kesho yanaandaliwa leo na usifikiri Kuna muda wa ziada Mungu atakupa WAKATI NDO HUU USIUCHEZEE, Huwa muda mwingine nafikiria hivi unautumia vizuri wakati huu ambao uko na nguvu?, kama huutumii vizuri kubadilisha maisha yako siku ukiukosa utakuja kujuta

Hebu jiulize mara ngapi umekutana na fursa na hadi leo hujaanza kuifanya eti unasubiria kazi zipungue ofisin, unasubiri upate mtaji mkubwa, unasubiri upate muda mwingi ndo uanze usije tegemea hayo yatatokea kwenye maisha yako na utakuwa unajipotezea muda wako, Anza leo maana wakati ndo huu ukishaona sehem ambayo utajifunza kitu, utaanzisha kitu usisubiri kesho, usisubiri uwe na muda wala pesa nyingi usisubiri umuone rafiki yako kufanya ndio na wewe ufanye Anza leo. Hebu angalia mwaka unaisha ulipanga nini na nini na nini kimetokea umekamilisha malengo yako.

UNAWEZA KUTUMIA MUDA KUPATA PESA LAKINI HUWEZI KUTUMIA PESA KUPATA MUDA, WAKATI NDO HUU JIPANGE

*** Emmanuel Mputa ***
The right action = Success
Phone:- 0717962720
           :- 0767962720
           :- 0628358487

Comments

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

ZIJUE SIKU HATARI KWA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO[MIMBA]