TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

Ninamshukuru Roho Mtakatifu yeye anipaye hekima na maarifa haya ya kufundisha Neno la Mungu.
Watu wengi huwa wanaisi kua dhambi,makosa na uovu ni kitu kimoja,sio kweli kibiblia.
KUTOKA 34:7a.Mwenye kuwaonea huruma watu elfu,mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi;
M.WALAWI 16:21a. Na Haruni mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israel na makosa yao naam,dhambi zao zote...
Hivyo tunaona kua kuna tofauti kati ya ivyo vitu..
Dhambi huu ni uasi.Ili kiebrania ni Chattah ni kwenda kinyume na kupungukiwa.ndio maana biblia inasema ni uasi
1YOHANA 3:4 Kila mtu afanyaye dhambi,afanya uasi maana dhambi ni uasi.
Ivyo dhambi ni kuvunja sheria ya Mungu,maana baada ya Mungu kutoa amri 10 alileta utisho na kusema wasifanye dhambi maana kuvunja amri ndio dhambi.
KUTOKA 20:20 Musa akawaambia watu msiogope,maana Mungu amekuja ili awajaribu na utisho wake uwe mbele yenu ili kwamba msifanye dhambi.
Makosa ili neno Kiebrania ni Pesha,Kutenda dhambi kwa kukusudia mtu anadhamiria kufanya kitu akijua ni kinyume.hii haijazungumziwa sana katika biblia.
UOVU/MAOVU.Hii ndio nguzo kuu ya anguko la kanisa na wakristo leo.
Kiebrania neno ili ni AVON,hii ni dhambi iliyo komaa au kujirudiarudia yani mtu kila siku anatenda dhamb na hayuko tayari kubadilika kuacha.
MARKO 7:21-22 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya,uasherati,wivu,uuaji,uzinzi,tamaa mbaya,ukirofi,hila,ufisadi,matukano,kiburi,upumbavu.23 Haya yote yaliyo maovu yanatoka ndani nayo yatia mtu unajisi.
Kumbe hayo matendo yote ni unajisi na ndio uovu.
HESABU 14:11,27 Bwana akamuuliza watu hawa watanizarau hata lini? wasiniamini hata lini? 27 Je nichukuane na mkutano mwovu mwovu huu uninung'unikiao hata lini?
AYUBU 34:36ab,37a Kwa kuwa umejibu kama waovu,kwani huongeza uasi juu ya dhambi zake.
KUTOKA 32:9,12b,14 Tena Bwana akamwambia Musa,Mimi nimewaona watu hawa,na tazama  watu wenye shingo ngumu.12b Geuka katika hasira yako kuu ughairi uovu ulionao juu ya watu wako,14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema atawatenda watu wake.Kumbe hapa tunaona hata Mungu akitenda kitu kibaya kwa watu wake ni uovu pia.
Utagundua sehemu kubwa ya watu kuangamia ili ni uovu soma
HESABU 14:34
ZABURI 31:10
EZRA 9:7
ZEKARIA 3:4
Watu wengi wanaangamia kwa ajili ya uovu walio nao lakini Mungu yeye husamehe uovu,yamini ukajiona uko sawa lakini kumbe umejaa uovu,Mungu usamehe
EZEKIEL 18:27.Tena mtu mwovu atakapoghairi na kuacha uovu wake alioutenda na kutenda yaliyo halali na haki,ataponya roho yake nayo itakua hai.Jichunguze moyo wako na utubu uovu wako ili uiponye roho yako.
Somo lakesho litakua sheria ya dhambi.
NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANIPAYE NGUVU

Comments

  1. Umenisaidia happy kwakweli nilikuswa sielewagi

    ReplyDelete
  2. Asante sana nimeelewa maana ya uovu.

    ReplyDelete
  3. Umetupea mifano kibibilia lakini hujatufafanulia kinagaubaga ndio tuelewe vizuri na kwa udani zaidi

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

Madini ya Zink na Ugumba