UANDAAJI CAKE
CAKE SIMPLE YA CHOCOLATE :
Kwa hisani ya laylbakes
Mahitaji:
🔸Unga wa ngano vikombe 2
🔸Sukari vikombe 2 unaweza punguza kidogo
🔸Cocoa 3/4 kikombe
🔸Baking powder vijiko 2 1/4 vya chai
🔸Baking soda 1/2 kijiko cha chai
🔸Chumvi kijiko 1 cha chai
🔸Maziwa ya maji kikombe 1
🔸Mafuta ya kula 1/2 kikombe
🔸Vanilla kijiko 1 1/2 cha chai
🔸Mayai 2
🔸Maji moto 3/4 kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA:
Hatua ya 1:
1. Washa oven joto 180°C. Paka chombo chako cha kuokea mafuta au siagi. Weka pembeni
Hatua ya 2:
2. Changanya mahitaji yote A katika bakuli kisha piga vizuri hadi mchanganyiko uwe laini
Hatua ya 3:
3. Tia Maji moto kisha piga tena kidogo tu kuchanganya. (Mchanganyiko wa keki utakuwa mwepesi usihofie)
Hatua ya 4:
4. Mimina mchanganyiko wako katika chombo ulichoandaa kisha oka kwa muda wa dk 30-50 au hadi kiasi ukichoma kijiti kati kinatoka safi. (Unaweza oka kwa mkaa pia)
Hatua ya 5:
5. Toa na wacha keki ipoe katika tin kwa dk 10 kisha toa ipoe kabisa. Ikishapoa pambia upendavyo. Enjoy !
#BYMALKIAWACAKE
Comments
Post a Comment