NETWORK MARKETING (BIASHARA YA MTANDAO)
IJUE BIASHARA YA MTANDAO(NETWORK MARKETING) NA FAIDA ZAKE.
Nawasalimu Ndugu zangu na Kuwakaribisha katika ukurasa huu wa Forever Living Products.
Naam karibuni sasa tushirikiane katika mada hapo juu.
Wengi huenda sio mara ya kwanza kusikia juu ya biashara ya mtandao(Network Marketing). Kama tunaijua twendelee kuijua zaidi, na kwa wale ambao ndio Mara yao ya kwanza kusikia, basi tufuatane hadi mwisho wa makala hii ili tuijue, karibuni.
Network Marketing(Biashara mtandao) ni biashara inayofanyika kwa kuwaunga zaidi watu kusambaza na kuuza bidhaa za kampuni kama wasambazaji ambao hulipwa kulingana na utendaji kazi wa mtu binafsi. Aina hii ya biashara huwa na kampuni linalozalisha bidhaa Fulani na kuziuza kwa kutumia wasambazaji waliokubaliwa na kampuni, ambapo wasambazaji hulipwa kamisheni kulingana na mauzo, lakini pia kupata faida fulani(retail profit) katika bidhaa hizo anapoziuza kwa mtumiaji wa mwisho. Hivyo msambazaji(distributor) anapouza zaidi ndipo kampuni nalo linapouza zaidi na kupata faida. Mfano mzuri wa network marketing ni kama wauzaji wa laini za simu wanavyopatikana na jinsi wanavyolipwa wasambazaji.
Makampuni mengine huuza bidhaa za vyakula, tiba lishe, madawa ya meno, bidhaa za mitindo, vifaa vya vyombo vya umeme(accessories), urembo(cosmetics) bidhaa za arts na aina mbali mbali za bidhaa zinazozalishwa na makampuni mbali mbali. Mfano wa hayo makampuni yanayofanya biashara zake kwa njia ya mtandao(network) ni kama FOREVER LIVING.
FAIDA ZA BIASHARA MTANDAO (NETWORK MARKETING).
1. UHURU WA MUDA/FLEXIBILITY OF TIME.
Katika biashara mtandao, Faida na sifa mojawapo kubwa ni Uhuru wa kutumia muda. Wote tunajua kuwa katika maeneo mengi ya kazi huwa na ratiba ya kazi ambapo mwajiriwa hutakiwa kuwasili kazini na kuondoka kazini. Hivyo kulisimamia hilo vizuri kunakuwa na mahali pa kusaini, mfano daftari la mahudhurio la wafanyakazi. Hapo unakuwa unaongozwa na muda uliwekwa na mwenye ofisi au taasisi hiyo maana ndiye boss wako. Hivi sivyo katika biashara ya mtandao. Katika network marketing hakuna mahali unapotakiwa kuripoti na kusaini uwepo wako kazini, hakuna boss wa mwenzake, kila mtu ni boss. Kila kitu kinategemea kujitoa kwako mwenyewe katika ratiba yako mwenyewe. Watu wengi sana katika biashara hii, wateja wao ni wale watu wa karibu yao, kama vile ndugu, marafiki na watu wanaofanya nao kazi au kuwasiliana kwa njia yoyote ile. Hivyo basi unaweza kuuza bidhaa muda wowote na mahali popote bila kuathiriwa na ratiba maalumu(fixed time schedule).
Zaidi kwa kuzingatia ratiba yako, unaweza ukawa na muda mwingi wa kutosha kukaa na familia yako, hasa watoto wako badala ya kuwaachia mayaya( house girls & houseboys). Hili haliwi rahisi kwa mtu anayeongozwa na ratiba ya ofisi, ndio maana wengine hufanya kazi siku zote saba za juma.
2. UHURU BINAFSI.
Fikiria hakuna boss ambaye unawajibika kwake, unakuwa boss mwenyewe, unatengeneza mtandao wako mwenyewe, wewe ndiye mwenye maamuzi ya kwanza na ya mwisho, unaamua upate fedha kiasi gani na kwa wakati gani. Hivyo unakuwa na uhuru wako binafsi ambao utakusaidia kufanya shughuli zako zingine nyingi.
3. FURSA KUBWA ZA MAFANIKIOWatu wengi wamekuwa mamilionea kupitia network marketing . Kwa kujitambua, nidhamu katika biashara na fedha, mafunzo na mtazamo sahihi kila mtu anauwezo mkubwa wa kufanikiwa katika biashara mtandao. Hivyo basi ukitaka kufanikiwa kiuchumi kwa kupitia network marketing, ni wewe kuwa utambuzi binafsi, nidhamu katika biashara na mawazo chanya ya kufikia ngazi za juu zilizowekwa na kampuni husika kulingana na mauzo yako.
4. FURSA ZA MAFUNZO BURE.
Kama tujuavyo, wengi tunakuwa na matamanio kufanikiwa kimaisha, tunaweza tukawa na mitaji mikubwa au midogo, lakini tusijue namna ya kuendesha biashara yoyote, na hata pale tunapojaribu kuanzisha jambo ya kututoa kimaisha tunaishia kupata hasara, kupoteza mtaji na kuilisika. Katika network marketing, mafunzo mbali mbali yahusuyo biashara ya mtandao, hutolewa bure ili msambazaji aweze kuimudu biashara aamuapo kujiunga mayo. Mafunzo yanakuwezesha kujua zaidi kuhusu bidhaa zitolewazo na kampuni, mfumo wa masoko(market plan), namna ya kupata kamisheni, faida ya papo hapo( retail profit), na mafunzo ya uongozi katika biashara. Hivyo uwezekano wa kufanikiwa zaidi unakuwa wa uhakika kwa distributor yeyote
5. MPANGO RAHISI WA BIASHARA/EASY BUSINESS PLAN
Mfumo wa biashara mtandao ni rahisi Sana, hauhitaji ujuzi fulani maalumu au masomo Fulani mahususi ili kuweza kuifanya hii biashara. Haihitaji matangazo maalumu kutangaza bidhaa zako, wasambazaji ndio huitangaza kwa kutumia midomo yao wanaponadi bidhaa lakini pia kutokana na ubora wa bidhaa, walio nunua huwa mabalozi kwa wengine na hivyo kufahamisha na kujulisha zaidi uwepo wa bidhaa hizo sokoni. Aidha hutolewa vipeperushi, vitabum DVD na CD na aina zingine za maandishi kuelezea bidhaa, hivyo msambazaji au mtu yeyote anayekuwa katika biashara hii huokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kwa ajili ya matangazo mbali mbali mbali.
6. KUFANYA BIASHARA UKIWA NYUMBANI/WORK AT HOME
Biashara hii haihitaji eneo fulani maalumu la kufanyia biashara. Mtu anaweza kufanya biashara hata akiwa nyumbani, maadamu tu anaweza kutumia internet, simu au kifaa chichote cha mawasiliano. Ni rahisi sana, kazi yako ni JUZA UZA ,yaani wajulishe wengine uuze bidhaa zako. Huu ndio upekee na urahisi wa biashara ya mtandao ukilinganisha na biashara zingine. Zinawafikia watu wengi kwa muda mfupi. Unaongea kwenye simu na wateja wako na mahitaji yao. Whatsapp, email, Facebook, twitter, YouTube instagram, telegram na aina zingine za mawasiliano , watu wengi hupata taarifa za bidhaa zako kwa muda mfupi lkn wewe ukiwa tu nyumbani na hivyo kuuza bidhaa kabla hata hujaonana na mteja.
7. KUTOKUWA NA MIPAKA NA RAHISI KUIENDESHA
Biashara mtandao haina mipaka kutokana na njia zake zinazotumika kuuza bidhaa. Mipaka ya mataifa, na kijiografia inaondoshwa katika biashara hii. Haina gharama za kuajiri wafanyakazi wengi ofisini na kukodi fremu za kuuzia. Mtaji wake ni Mdogo sana kuweza kuingia katika hii biashara ukilinganisha na biashara zingine nje ya mfumo huu. Kumbuka unaweza kuifanya na kuisimamia hii biashara hata ukiwa nyumbani kwako.
8. KUPATA MSHAHARA/KIPATO CHA ZIADA(Getting passive salary).
Faida na sifa nyingine ya kipekee ya biashara hii ya mtandao ni kuweza kupata kipato kingine cha ziada mbali na kile upatacho katika uajiriwa wako. Unaendelea kufanya kazi yako ya kila siku na kupata stahiki zako kama kawaida huku ukiwa nako unaingiza kipato kingine bila kuathiri kazi yako. Kumbuka hii biashara hufanyika mahali popote na muda wowote. Wengine hupata kipato kikubwa zaidi ya kile wanachikipata katika mishahara yao ya kawaida. Hilo huwafanya wengine kufikia hatua ya kuacha kazi zao rasmi na kuisimamia biashara yao ya mtandao.
9. KUENDELEA KUPATA KAMISHENI HATA KAMA UTASIMAMA KWA MUDA KUSAMBAZA BIDHAA.
Biashara ya mtandao ni ya kuunganishana, kutengeneza kama mnyororo ambapo anayekuunganisha anapata kamisheni ya point za kuunganisha distributor mwingine, mauzo yake binafsi na mauzo ya watu aliowaunganisha. Kwahiyo the more you join the others the more you get more commission ! Hivyo unaweza ukaumwa usipate kuuza bidhaa zako, lkn wale uliowaunganisha wakiuza kwa upande wao, wewe pia unapata points za kamisheni kutoka katika mauzo yao. Na unapowaunganisha zaidi na kuuza ndipo cheo chako katika mtandao kinapandishwa na malipo yako kuwa makubwa zaidi.
10. NI BIASHARA YA MAISHA YOTE.
Sifa nyingine ya biashara ya mtandao, ni kwamba ni ya maisha yote(KWA BAADHI YA MAKAMPUNI). Ukijiunga na hii biashara unaweza kuendelea nayo maisha yako yote kwa angalau kununua bidhaa mara moja kwa mwaka mzima. Biashara hii kwa kampuni fulani nilijualo hurishishwa hata kwa watu walio nyuma yako, ikitokea maisha yako au uwezo wako wa kuendelea nayo umefika, basi utamrithisha mrithi wako kuendelea nayo. Hivyo uwezekano wa kuipoteza biashara hii au kufilisika ni mdogo sana ikifanywa kwa nidhamu na malengo.
Kwa leo ningependa nikomee hapa maana faida ni nyingi sana, zikiwemo za kusafirishwa nje ya nchi, tours za hapa na pale na mambo mengine yanayojili katika biashara nini. Aidha Nitoe rai, si makampuni yote yanayofanya network marketing ni bora na kwamba yanaweza kukutoa kimaisha. Wengi bila kufanya tafiti za kina kuhusu ubora wa kampuni, bidhaa zake na mfumo wa malipo yao, wamejikuta wanaingia kwenye hii biashara kwa kwambiwa inalipa pesa nyingi kwa muda mfupi, lkn mwisho walipojiunga wakajikuta wanabaki na bidhaa ndani, hawapati wateja na kuopoteza fedha zao bure. Mfano mengine hadi ufikie mauzo ya point kadhaa ndipo ulipwe, wakati mengine hata point moja unalipwa. Hivyo umakini mkubwa unahitajika kujiunga na hii biashara.
Kwa kuijua zaidi na ushauri kuhusu kujiunga na biashara ya mtandao(network marketing), tunaweza kuwasiliana kwa namba ntakazo weka chini ya makala nini.
NB: BIASHARA HII HAIHITAJI UCHOYO, UNAPOJIUNGA HAKIKISHA UNAMSAIDIA NA MWENZAKO KUWEZA KUJIUNGA ILI KUFANIKIWA KWA PAMOJA NA KUUSHINDA UMASIKINI.
kwa mawasiliano zaidi.piga/SMS/WhatsApp
+255767962720 au +255625748804
Comments
Post a Comment