ASETS AND LIABILITY

*ASSET AND LIABILITY*

*Asset* ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

*Liability*ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri,hiki ndio kitu pekee  unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.
Matajiri wote wananunua Assets,lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kua ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama,nyumba,gari,simu,laptop, duka.
Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa,lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba,kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana,maana haikuingizii hata mia,badala yake inakutolea pesa,utalipa umeme,maji,ukarabati na malekebisho ya vitasa,taa,furniture n.k,hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha,hiyo ni Asset. Gari,kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa,itahitaji mafuta,service,na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi,ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchart,hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia,maana siku umelifunga huingizi chochote,matumizi yoote unategemea dukani,badala ya duka kukupa faida,unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiliwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV,radio,simu kubw,gari,fridge,nguo,viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine,mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao,badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara(Income) ukiongezeka,matumizi(Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa dalasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato(Income) na kupunguza upande wa matumizi(Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities,wananunua Luxuries kama gari,tv ,sm kubwa  pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida,hivyo faida ndio inanunua magari,nyumba,TV nnk, ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili,lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka.
Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

*Wealth* is a person's ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today,how long could you survive?
Maana yake,kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato,una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani??
Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.
Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities, na pia ujiulize are you Wealth or not?

Comments

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

Madini ya Zink na Ugumba