UTUMBO KUZIBA
Utumbo kuziba Iwapo kuna kitu ambacho kimeziba sehemu yoyote ile ya utumbo, chakula na kinyesi haviwezi kupita. Hii inaweza kusababisha maumivu na maambukizi. Pamoja na maumivu, mtu huyu anaweza kuanza kupata choo kigumu au kutopata choo kabisa na kutapika. Tumbo linaweza kuwa kimya, au kutoa sauti nyingi zenye mlio wa juu. Uzibe utumboni huweza kusababisha kutapika kwa nguvu. Tatizo la utumbo kuziba linaweza kusababishwa na: Fungu la minyoo lililojisokota kama mpira . Henia . Sehemu ya tumbo kujisokota kutokana na kovu la zamani. Hii inaweza kumtokea mtu ambaye aliwahi kupata jeraha au kufanyiwa upasuaji kwenye utumbo. Saratani . Kama unadhani kuna uzibe kwenye utumbo, fanya mambo 2: Mpeleke mgonjwa hospitali mara moja. Huenda upasuaji ukahitajika. Kama kuna minyoo mahali unapoishi, mpe dawa ya minyoo ya askarisi ukiwa unampeleka hospitalini, hasa kama minyoo ndiyo itakuwa imesababisha uzibe huo. Bonyeza hapa kwa ajili ya dawa za minyoo . Ugonjwa wa kidole tumbo na uvi...