Posts

Showing posts from December, 2016

SIKILIZA: CHANZO CHA SIKUKUU YA KRISMASI

Image
Kila tunapokaribia sikukuu ya Krismasi, watu wengi wanauliza maswali juu ya chanzo cha Sherehe hii ya Krismasi ya tarehe 25 Desemba katika Ukristo, hivyo nimeona nitoe majibu ambayo naamini yatawasaidia wengi wanaopenda kuujua ukweli. Maswali: Ni nini Chanzo cha sikukuu ya Krismasi ya tarehe 25 Desemba? Je ni kweli Yesu alizaliwa tarehe hiyo? Ilianzaje na ilianza lini kusherekewa na Wakristo? MaJibu: Kwa mujibu wa Biblia, wakristo wengi wanaamini kuwa Yesu alizaliwa, ila hakuzaliwa tarehe 25 Desemba, na hakuna sehemu yoyote ya biblia inayotaja tarehe ya kuzaliwa Yesu, wanafunzi wa Yesu pamoja na Kanisa la Kristo waliloliacha mitume hawakuwahi kusherekea sikukuu hii ya Tarehe 25 Desemba kama siku ya Kuzaliwa Yesu Kristo. Tunapochunguza Biblia tunaikuta tarehe 25 December, kuwa ni sikukuu iliyokuwa inaadhimishwa na wapagani wa Babeli ambako Waisraeli walichukuliwa mateka. Hivyo sikukuu ya 25 Desemba ilikuweko kabla ya Kuzaliwa Yesu, na ilikuwa sikukuu ya wapagani wa Babebli wakishereheke...

NI HALISI NA HAZINA MADHARA YOYOTE KWA MTUMIAJI….. HISTORIA FUPI

 Bidhaa za Foreverliving zimeanzishwa na Bwana Rex Maugan ambaye ni mtu hodari na aliyekuwa na ndoto. Kwa miaka mingi alikuwa akiwaza kuanzisha kampuni itakayo saidia watu afya na kipato.  Mwaka 1978 alifanikiwa kupata wazo na kualika watu 43 kushiriki mkutano wa kwanza huko Phoenix, Arizona. Mkutano ndio ulikuwa chanzo cha kuanzisha kampuni ya ‘Foreverliving products’ iliyosambaa nchi zaidi ya 130 duniani na kufanikisha ndoto yake. MALIGHAFI Bidhaa za Foreverliving hutengenezwa kwa kutumia mmea aina ya Aloe Vera na Asali ya nyuki wadogo. Mmea wa Aloe Vera ni moja kati ya mimea ya dawa iliyojulikana tangu kitambo sana.  Una zaidi ya miaka 2000 katika historia na Sayansi. Kuna zaidi ya aina 200 za mimea ya Aloe Vera . Mmea wa Aloe Vera una zaidi ya virutubisho 75 ikiwa ni pamoja na madini 20, amino acid 18 na vitamin 12. Aloe Vera ina uwezo wa kupenya mwilini na kufikia tishu za ndani kabisa, tabaka saba kwenda ndani. Bidhaa za Foreverliving hutumia aina moj...

LIPA GHARAMA ILI UFANIKIWE

Image
Habari za Leo Rafiki. Natumaini Unaendelea Vyema sana. Mimi pia nipo Vyema. Kwenye safari yetu ya mafanikio kuna vitu vingi tunafanya ili tusonge mbele kila wakati. Ili mtu atoke sehemu moja aliyokuwepo na kusogea mbele anahitaji gharama.  Sio kitu kirahisi kama unavyoweza kufikiri ndio maana sio wote wanaweza.  Watu wengi huingia kwenye biashara au huanza vitu vipya na kutegemea matokeo bila kulipia gharama yeyote. Kama ilivyo kwa Mtoto anavyozaliwa ili aweze kupitia hatua za ukuaji anahitaji kulishwa chakula bora na vilevile matunzo ya kutosha. Haiwezekani mtoto akizaliwa leo aachwe hovyo hovyo halafu tutegemee akue kirahisi lazima ataugua na mwishoe kufariki. Hivyo pia kwenye vitu tunavyofanya tunahitaji uvumilivu,  kujifunza, kufanya kazi kwa bidii, muda wa kusubiri matokeo. Haitokei tu ghafla ukaanza kuona matunda ya mti. Lazima zipite hatua mbalimbali hadi uone matunda. Hata unapootesha nyanya ukaziacha shambani bila kuzihudumia usitegemee mabadiliko yeyote. Zaidi u...