SABABU ZINAZOPELEKEA MTOTO KUTOKUCHEZA TUMBONI
Mama mjamzito huwa anasikia raha pale mtoto anapoanza kumpiga piga tumboni kwa mara ya kwanza, kucheza kwa mtoto kunafanya kuwa na mawasiliano mazuri kati ya mama na mtoto .Kwa wenye mimba ya kwanza mtoto ataanza cheza wiki ya 24 miezi (5-6), ila kwa wale walio zaa tayari mtoto mmoja au zaidi wanaskia mtoto akicheza akiwa na wiki ya 18-22 mapema kidogo.
Kuna umuhimu wa mama kufatilia kujua kucheza kwa mtoto,kwa kawaida watoto wanatakiwa wacheza mara 6 -10 ndani ya lisaa limoja (1hr) ile miezi 3 ya mwisho,na ile miezi 6 ya mwanzo kucheza kwake sio sana. Cha muhimu unatakiwa ujue pale anapocheza na asipocheza.Kipindi cha usiku ndio muda wa watoto kupigapiga kuliko mchana ,na baada ya mama kula chakula pia huwa wapiga piga sana tumbo.
Sababu zinazompelekea mtoto kuto kucheza
: Mtoto kukosa nguvu za kutosha kutokana na lishe mbaya ya mama yake
:Mtoto hapati hewa ya kutosha kutoka kwenye placenta
:Mtoto kuwa mdogo sana na uzito mdogo nayo unamfanya ashindwe kucheza au akacheza kwa mbali sana na kukufanya wewe usimskie kama anacheza.
:Mama anapokuwa na maradhi au matatizo ya kiafya, hudhoofisha afya ya mtoto na kukosa nguvu
:Mama anapokuwa amechoka sana kwa safari au kazi ngumu ,mtoto nae anakuwa anachoka na kuhitaji kupumzika na huwa kimya sana
:Mama anapotembea sana au kusimama kwa muda mrefu,kuna mfanya mtoto analale na kumfanya asicheze .
NJIA ZA KUMFANYA MTOTO ACHEZE TUMBONI
Mama anapohisi mtoto yupo kimya anaweza
:Kunywa maji baridi sana
:Kunywa juice
:kaa sehemu yenye makelele kama ya radio,tv au washa vacuum cleaner
:Kula chakula au snacks -ataanza kucheza
:Lala ulalie ubavu wa kushoto
:Kaa chini na unyooshe miguu juu ya kitu
Iwapo ukatumia njia zote hizo na bado yupo kimya ni vizuri ukawahi hospital ,iyo ni ishara mbaya.
NB. MTOTO ANAPOJINYOOSHA MWILI, KUKUNJA MGUU AU MKONO KUNAWEZA MSABABISHIA MAMA KUPATA MAUMIVU ,UNATAKIWA KUPAKA MAFUTA YA MAJI TUMBONI NA KULIFANYIA MASSAGE ATAJIGEUZA NA MAUMIVU YATAISHA
Kwa ushauri +255767962720
Comments
Post a Comment