NI NAMNA GANI UNAWEZA KUWA NA UHUSIANO WA KUDUMU MUDA MREFU NA WENYE FURAHA TELE
Habari za leo ndugu mfuatiliaji wa JITAMBUE,natumaini ni mzima wa afya njema.karibu tena katika ukurasa huu wa KUJITAMBUA,leo napenda kuongelea namna tunavyoweza kuwa na uhusiano imara na wa muda mrefu na wenzi wetu,kila mwanadamu mwenye hisia anapenda siku moja kuwa na mwenza sahihi atakayeishi nae muda mrefu katika maisha yake yaliyosalia hapa duniani katika uhusiano wenye furaha na mapenzi tele .Lakini asilimia zaidi ya 70% wengi tumejikuta tukiiishia katika uhusiano wa muda mfupi tena uhusiano ukiisha kwa uhasama zaidi,hapa leo naongelea jinsi ya kujenga mahusiano ya muda mrefu,wakati mwingine nitaongelea ni namna gani unaweza kumchagua mwenza sahihi.Asikudanganye mtu maisha ni matamu pale unapokuwa na mweza sahihi katika uhusiano ulio bora,dunia yote utaiona ya kwako.Weng wetu tumekuta uhusiano wetu ukifa kwa kutojua njia au namna sahihi ya kuishi na wapenzi wetu,uhusiano sio jambo dogo sio jambo linalokwenda tu hivi hivi lenyewe,uhusiano au Ndoa bora unajengwa kila siku,kupendana ni jambo moja na kuishi kwa kupendana kwa muda mrefu ni jambo la pili,mnaweza mkapendana kabisa lakini mkashindwa kuishi pamoja,haya ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia kujenga uhusiano wa muda mrefu kwa mpenzi wako.
1. KUWA NA IMANI NA MPENZI WAKO
Uamnifu ni jambo pana katika uhusiano, na ndio unajenga uhusiano au ni msingi wa kuwa na uhusiano bora na wa muda mrefu.Uaminifu unajengwa mwanzoni kabisa wa uhusiano wenu,mwanzoni kabisa mwa mauhusiano jenga uaminifu kwa umempandae,mwanini hajakupenda kwa bahati mbaya na anakupenda kwa dhati ,lakini ili ujenge uaminifu na wewe pia lazima ujiamini,Jiamini wewe ni mtu sahihi kwake,usiwe na mashaka na hofu,mara nyingi watu tumekuwa na hofu mioyoni mwetu na ndio sababu kuwa ya kutoaminiana.Una hofu na mpenzi wako kwa kila kila kitu iwe anachoongea au anachokifanya,akikwmabia I love youunaona kama anakudanganya,akichelewa sehemu kurudi unahisi alikuwa na mpenzi mwingine hata akikupa sababu za maana ,wewe huelewi zaidi utamjibu wee endelea kunifanya mjinga tu,ukimwona yupo na mtu unahisi wanatongozana,kila anachofanya huna imani nae.Kama huna imani mapenzi hugeuka kuwa msalaba mchungu kwako kila muda wewe moyo uankuenda mbio,ukimpgia simu hata mchana inatumika kwako kosa,akijakupokea jambo la kwanza naona unaongea na hawara zako?.Kuwa na imani na mpenzi wako lakini pia kuna njia za kujijengea imani katika penzi lenu.Katika makala nyingine nitakuja kuongelea ni namna gani mnaweza kujenga imani katika penzi lenu.
2. MATENDO YAWE MENGI KULIKO MANENO
Katika uhusiano ni jambo la msingi zaidi katika kuboresha uhusiano ni matendo zaidi kuliko maneno.Usiishie tu kusema I LOVE YOU ya mdomo,hakikisha hiyo I love you iendane na matendo ya kumaanisha kweli unampenda,mfanyie mambo yatakayodhihirisha unampenda na kumjali.Jaribu Kumsoma mpenzi wako nini anapenda na kadri uwezavyo hakikisha unamfanyia yale anayoyapenda na kumfurahisha
Itakuwa ni jambo la kustaabisha upo na mpenzi wako muda wa miaka mitatu lakini huju anapenda nini?unaweza kukuta msg nyingi I MISS YOU SO MUCH lakini kweli ukikutana nae unaonyesha ulimmiss? Unaweza kukuta mtu na mpenzi wake hawajaonana muda mrefu lakini wakikutana wanaangaliana kama mtu na kaka yake,mwonyeshe mpenzi wako ulimmmiss,mkumbatie mpenzi wako unamwogopa nani? Usoni kweli uonyeshe ni ni namna gani ulimmiss.
3. KUSHIRIKIANA KATIKA KILA JAMBO.
Kushirikiana ni jambo la msingi zaidi kwa wapendanao.Jinsi mnavyoshirikiana ndio jinsi mnavyozidi kujiweka pamoja zaidi,mshirikishe mwezi wako mawazo yako,mipango yako na mara nyingi usifanye maamuzi bila kumuhusisha mwenzi wako labda yale maamuzi ya binafsi sana ndio unaweza kufanya peke yako.Kama kuna jambo mnaweza kufanya pamoja ni vizuri mkafanya pamoja kama matembezi ya jioni kwa pamoja,kusafiri pamoja,kufanya mazoezi pamoja wakati mwingine hata kupika pamoja.Mambo mengine unaweza kuona ni madogo lakin yanaimarisha uhusiano kwa kiwango kikubwa kwa wapenzi kujiona wamoja.Kuna tatizo huwa linajitokeza hapa katika kushirikiana maswala ya msingi baada ya mmoja kumuona mpenzi wake hana sifa Fulani,kwa mfano mume ni profesa mke kaishia form four,hapa mume huona mke wake hana cha kumshauri kutokana na tofauti kubwa kielimu,ndugu yangu uprofesa wako ni nje ya nyumba ndani wewe ni mume wadhifa wako unauvua mlangoni.Hivyo hivyo mmoja akijaliwa pesa sana kuliko mwenzie tatizo la kushirikiana huwa kubwa zaidi.
4. NAMNA MNAVYOSULISHISHA MIGOGORO PALE INAPOJITOKEZA
Hakuna usiano usio na mikwaruzo au mogongano ya hapa na pale na pale,hilo ni jambo lisilokwepa kwa wapendanao,ni lazima kutakuwa na kutoelewana wakati mwingine.Lakini kutofautiana haimanishi ndio mwisho wa mahusiano,kuna wakati mwingine baada ya matoelewano basi baada ya suluhu uhusiano huimarika zaidi na kuwa bora kuliko mwanzo.Jambo la msingi ni namna gani wewe na mpenzi wako mnatumia njia gani kutatua tatizo la kutoelewana. Wapendanao wenye ujuzi mdogo wa kutatua migigogoro huishia kupigana,kutoleana maneno ya kashfa,kuninuniana kwa muda mrefu. Wenye Uhusiano wenye mafanikio wanauwezo wa kusulisha matatizo yao na kuyamaliza bila kufikia hatua mbaya,hata kama wana hasira vipi basi kila mmoja wao hujitahidi kujizuia kuhakikisha suluhu inapatikana,pale suluhu inapopatikana husamehe na kusahau.Na kila siku hujifunza kukua katika kutatua tatizo pale kunapotokea kutoelewana baina yao. “ Like fine wine, their relationship improves with age and gets better over time”
“The group with whom I’ve always been most fascinated is the one I call ‘marital masters’ – folks who are so good at handling conflict that they make marital squabbles look like fun. It’s not that these couples don’t get mad and disagree. It’s that when they disagree, they’re able to stay connected and engaged with each other. Rather than becoming defensive and hurtful, they pepper their disputes with flashes of affection, intense interest, and mutual respect.”-John Gottman.
“Let the little things go. People who struggle often fight over little things. We obsess over things that don’t really matter. We create resistance instead of letting things glide off us. Let the little things go, breathe, and move on to the important things.”-leo Baubauta
Itaendelea usikose kuisoma hapa
Kumbuka taaluma uliyonayo,cheo ulichonacho au fedha ulizonazo haziwezi kufanya kuwa na uhusiano wakudumu na wenye furaha.Mapenzi ni ujuzi unaotakiwa kuutafuta.
JITAMBUE SASA
+255767962720/+255717962720
Comments
Post a Comment