SOMO MUHIMU JIJUE
UJUMBE WA LEO
Kuanza kuchepuka kwa mwanamke ndani ya ndoa, huanza kwa mwanaume, ukiwa mchepukaji, mke naye baadaye anaweza kuwa mchepukaji.
Mwanaume unamwambia mkeo awe mwaminifu, je wewe mwaminifu? SIyo unamwambia yeye awe mwaminifu halafu kumbe una vimada kadhaa nje ya ndoa, sasa kwa nini yeye awe mwaminifu na wakati wewe siyo mwaminifu?
Mwanaume anasema kwamba anataka kuoa mwanamke bikira, sawa, ni vizuri, lakini je, wewe ni bikira? Je hujawahi kufanya mapenzi? Kama ndiyo, basi oa bikira, ila kama umewahi kufanya mapenzi, sioni sababu ya kuoa bikira.
Mwanaume unakwenda kuoga, ukisikia simu yako inaita chumbani, na mkeo yupo huko, tayari unaanza kuwa na wasiwasi, mpaka wengine wanatoka na mapovu bafuni kwenda kuwahi simu ili mke asijue nani anapiga.
Kama hujajiandaa kuoa, kama hujamaliza mambo yako, kama kila demu unataka kugonga, nadhani endelea kwanza, ukishamaliza mambo yako ndiyo uoe kwani vinginevyo, ndoa itakusumbua tu.
Kama hutaki kumwamini mkeo ndani ya ndoa, utamwamini nani sasa? Mwingine anamwambia mkewe kwamba lazima simu yake iwe huru, yaani hata yeye awe anatumia au kuangalia chochote muda wowote, je wewe yako ipo huru? Sio unamwambia yake iwe huru halafu yako unakuwa mkali.
SImu unaweka password kila kona, kuifungua, password, kuangalia picha, password, kusoma meseji, password, ni vizuri kama mkeo anajua password zote, ila ni vibaya kama mkeo hajui chochote kile.
Wengi tunatamani kuwa na watoto, lakini je tumejiandaa kupokea watoto? Ni vibaya na inaweza kuwa laana kama utamzalisha mwanamke na kisha kumuacha aendelee na maisha yake, wakati mwingine machozi yake yanaweza kuziba baraka zote Mungu alizotaka kukupa.
Mwingine anasema hawezi kutumia mpira kwa kuwa ladha inapungua, hakuna kitu kama hicho. Unapokaa kijiweni, watu wanapokwambia kwamba kondomu zinapunguza ladha, ubongo wako unapokea taarifa hizo na kuzihifadhi, unapokutana na mwanamke, kitu cha kwanza ubongo unakukumbusha taarifa ile kwamba kondomu hupunguza ladha, hivyo mwili unakubaliana nao, na kweli ukifanya hupati ladha kwa kuwa ubongo unakuwa unafanyia kazi taarifa iliyopokea.
Wakati mwingine unakutana na demu mkali kwenye daladala, unamyumbisha, anakuelewa, usiku unakutana naye na kufanya naye bila kinga....Mungu atusaidie.
Vijana ndoa zetu hazikai kwa sababu tunataka tuwe Magufuli, yaani kurudi nyumbani kwa kushtukiza. SIkiliza, wazee wanasema ndoa zao zilidumu kwa kuwa hawakuwa wakimfuatilia mwanamke, anaporudi nyumbani na mzigo, kitu cha kwanza anamtuma mtu atangulize mzigo, lengo ni kumfanya mkewe ajue kwamba mumewe anarudi, hivyo kama kuna ujinga alikuwa akifanya, au sehemu yupo arudi. Ila sisi vijana, tunataka kushtukiza, mwisho wa siku, tunaumia kwa maumivu makubwa.
Ndugu yangu, kukosa kazi kunauma ila kuumizwa mapenzini hasa na mtu unayempenda, kunauma zaidi.
Wanawake wote hufanana...yaani hata awe mkurugenzi wa benk fulani, bado atakuwa vilevile. Hakuna utofauti kati ya mwanamke masikini wa kule kwetu Nyamkunga na mkurugenzi wa benki fulani, kitabua hufanana....mwanamke kuwa malaya na kupata tabia za kijinga hutokana na mwanaume....wewe ndiye utakayemfanya mke awe malaya, mwenye choyo, mchafu na tabia nyingine...ila kumbuka kwamba wewe ndiye utakayemfanya mwanamke kutulia na kuwa na msimamo.
Comments
Post a Comment