TOP TEN DISEASES IN TANZANIA
Maana ya Shinikizo kubwa la Damu: Ni ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini. Ukubwa wa shinikizo hilo la damu utegemea wingi na nguvu ya msukumo wa damu kutoka kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu mwilini. Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu. Dalili: Kwa kawaida hakuna dalili za wazi zinazojitokeza pale ambapo una shinikizo kubwa la damu. Utafahamu kama una shinikizo kubwa la damu kwa kupimwa na mtaalamu katika kituo cha tiba. Endapo shinikizo lako la damu litakuwa liko kiwango cha juu sana unaweza:
Muda wa tatizo: Kwa bahati mbaya watu wengi huishi na tatizo hili kwa muda mrefu bila kufahamu kwani hakuna dalili zilizo bayana. Mara nyingi shinikizo kubwa la damu hutambulika pale unapokwenda kituo cha huduma ya afya kupima afya yako au kupata matibabu ya tatizo jingine la kiafya. Hali hii humweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kupima afya yako mara kwa mara. Sababu: Sababu hasa za shinikizo kubwa la damu kwa sehemu kubwa hazijulikani. Hata hivyo shinikizo la damu hubadilika mara kwa mara kutegemeana na shughuli mtu anayofanya, hali ya joto, chakula alichokula, hali ya msongo wa mawazo, ukiwa umelala au kusimama na hata matumizi ya baadhi ya dawa. Watu wenye umri wa miaka 45 au zaidi wako kwenye hatari zaidi ya kupata shinikizo kubwa la damu kutokana na mabadiliko yanayotokea katika mishipa yao ya damu. Vilevile mafuta, lehemu au madini ya chokaa yakizidi mwilini huwa na tabia ya kujikusanya katika kuta za ndani za mishipa ya damu kidogo kidogo na kusababisha mishipa hiyo kuwa nyembamba na hivyo kupunguza uwezo wake wa kutanuka. Hali hii huchangia kwa kiasi kikubwa kupata shinikizo la damu. Viashiria vya shinikizo kubwa la damu: Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu ni pamoja na:
Nifanye nini kujiepusha na shinikizo kubwa la damu?
Madhara ya shinikizo kubwa la damu:
Matibabu:
************************************************************************************** 2. UGONJWA WA KISUKARI Ugonjwa wa kisukari ni nini? Ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda murefu. Sukari hutumiwa na mwili ili kupata nishati-lishe. Ili mwili uweze kutumia sukari inayotokana na chakula huhitaji kichocheo (hormone) cha insulin. Kichocheo hiki hutengenezwa na kongosho (pancreas). Kichocheo cha insulin ndicho kinachodhibiti kiwango cha sukari katika damu. Wakati kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulin au insulini iliyopo katika damu inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi husababisha ugonjwa wa kisukari. Aina za Kisukari Kuna aina mbili za kisukari:-
Viashiria vya kupata ugonjwa wa kisukari Mtu yeyote anaweza kupata kisukari, hata hivyo kuna mambo mengi yanayoweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari. Haya tunaweza kuyaweka katika makundi kutegemeana na aina ya kisukari:
Kisukari kisichotegemea insulin (type 2 diabetes) huhusishwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha usiofaa. Baadhi ya viashiria vya aina hii ni
Dalili za ugonjwa wa kisukari
Ukiona dalili hizi nenda kituo cha huduma ya afya upate ushauri na kupimwa ili kudhibitisha. Madhara ya ugonjwa wa kisukari
Dalil za awali
Dalili za kati
Dalili za baadae
Tahadhari: Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe kinywaji au chakula. Anaweza kuwekewa glukosi kidogo kati ya shavu na fizi. Awahishwe hospitali haraka iwezekanavyo.
Dalili za kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu ni
Madhara ya muda mrefu:
Kumbuka: Madhara ya muda mrefu huweza kuzuilika. Fata masharti unayopewa na daktari. Chakula kwa wagonjwa wa kisukari
************************************************************************************ 3. UGONJWA WA MOYO Ugonjwa wa Moyo ni nini? Ugonjwa wa moyo au magonjwa ya moyo yanahusisha yale magonjwa yoyote yanayoathiri moyo na mishia yake. Magonjwa ya moyo yanajumuisha coronary heart disease, myocardia infaction (heart attack), congestive heart failure, atherosclerosis, angina, cerebrovascular diseases, stroke (kiharusi), aneurysm na peripheral vascular disease. Sababu: Tafiti zimeonyesha kuwa ugonjwa wa moyo huanza pale ambapo mambo Fulani yanaposababisha sehemu ya ndani ya kuta za mishipa ya damu kuharibiwa. Mambo hayo ni pamoja na:
Kuta za mishipa ya damu zikiharibiwa, mafuta hujikusanya katika sehemu ya mishipa iliyoharibiwa na kutengeneza utando wa mafuta (plaque). Kadiri muda unavyoendelea ndivyo mafuta haya yanavyozidi kujijenga katika sehemu hiyo hadi kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba na hivyo kupunguza kiasi cha damu kinachobeba hewa ya oksijeni na virutubishi kwenda kwenye misuli ya moyo. Hatimaye sehemu hiyo ya mshipa inaweza kupasuka. Kama sehemu hiyo ikipasuka, sehemu ya seli za damu zinazoitwa platelets ambazo husaidia mwili kuponya kidonda hujigandisha kwenye mpasuko na hivyo kuanza kujikusanya. Hali hii huongeza mkusanyiko, hivyo kuendelea kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba zaidi na hali hiyo husababisha moyo kushindwa kufanya kazi na mtu hupata ugonjwa wa moyo (heart attack). Mkusanyiko wa mafuta na platelets wakati mwingine huweza kumeguka kama mabonge na kusafiri kwenda kuziba mishipa midogo ya damu ya kichwani. Hali hii ikitokea mtu hupata kiharusi. Hali ya kujijenga kwa mafuta na platelets hutokea polepole, huchukua muda mrefu na huweza kujitokeza kwa dalili kama kupanda kwa shinikizo la damu. Dalili za ugonjwa wa moyo: Mara nyingi hakuna dalili inayojitokeza mpaka pale moyo unaposhindwa kufanya kazi ghafla (heart attack), au mtu anapopata kiharusi. Zaidi ya hayo, dalili za ugonjwa wa moyo hutofautiana kutegemeana na aina ya ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, hazijitokezi mapema na kama zikijitokeza dalili za ugonjwa huu ni pamoja na:
Hadi mtu kuanza kupata dalili hizi amekuwa ameishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu. Hivyo, njia bora ya kugundua mapema dalili ya ugonjwa /magonjwa ya moyo ni kuchunguzwa afya yako mara kwa mara. Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo:
Mambo ya kufanya ili kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo
Ushauri kwa wenye ugonjwa wa moyo: Fuata kwa makini taratibu za matibabu kama ulivyoshauriwa na daktari ikiwa ni pamoja na:
*************************************************************************************
Ugonjwa wa UTI ni nini? UTI kitaalamu ni “Urinary Tract Infection” ni magonjwa au maambukizi yanayoathiri mfumo wa kutengeneza na kutoa mkojo nje ya mwili. Mfumo huu unahusisha kibofu cha mkoja, figo pamoja na milija inayounganisha kibofu cha mkoja na figo. Pindi wadudu yaani bacteria wanapoingia katika mfumo huu wanaweza kusababisha maambukizi ambayo mara nyingi wataalamu hupenda kuyaita UTI. Mara nyingi maambukizi ya mfumo huu wa mkojo huwa ni maambukizi ya kibofu cha mkojo (Bladder infections). Maambukizi ya kibofu cha mkojo kawaida hayana madhara makubwa kama yakitibiwa haraka. Yasipotibiwa yanaweza kusambaa hadi kwenye figo zako. Maambukizi ya figo yana madhara makubwa sana kwani huaribu figo ambapo unaweza kupata magonjwa ya figo ambayo tunayaita Kidney au Renal Deseases. Nini usababisha UTI? Kawaida Bakteria uingia kwenye mfumo wako wa mkojo kupitia kwenye mlija mdogo wa mkojo ujulikanao kitaalamu kama urethra mlija unayobeba mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo kwenda nje ya mwili. Bakteria wanaosababisha maambukizi uishi katika utumbo mkubwa wa chakula na upatikana kwenye choo au kinyesi. Mara nyingi bacteria hawa wanaitwa E. Coli. Bakteria hawa upitia kwenye urethra na kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo hadi kwenye figo na kusababisha maambukizi. Wanawake hupata UTI zaidi ya wanaume kwa sababu milija yao ya kutoa mkojo kwenye kibofu cha mkojo ni fupi zaidi ya wanaume na hivyo kuwezesha bacteria kusafiri kwa urahisi zaidi hadi kwenye kibofu cha mkojo. Pia kufanya tendo la ndoa au kujamiana pia kuna rahisisha bacteria kuingia kwenye urethra. Pia unaweza kupata UTI kwa kutokunywa maji ya kutosha kwani maji husaidia kutengeneza mkojo wa kutosha na hivyo unapokojoa unasafisha milija yako ya kutoa mkojo nje ya mwili. Pia watu wenye ugonjwa wa kisukari wana hatari ya kupata UTI mara kwa mara kwani kinga ya mwili hushuka na hivyo kusaidia kupata maambukizi kirahisi na pia mkojo anaotoa huwa na kiasi kikubwa cha sukari ambacho husaidia wadudu kukua vizuri. Pia mama mjamzito hupatwa na UTI zaidi. Uwezekano wa kupata maambukizi ni makubwa endapo unatatizo linalosababisha mkojo kushindwa kutoka nje ya mwili kama vile, mawe kwenye figo yaani kidney stones au ongezeko la tezi la kibofu cha mkojo yaan enlarged prostate kitaalamu BPH. Wanawake upata UTI mara kwa mara na hizi zinaweza kuwa sababu zinazoongeza uwezekano wa kupata UTI mara kwa mara:
Dalili za UTI
Matibabu: Nenda hospitali ili upimwe mkojo wako ili kugundua kama una UTI au maambukizi mengine kama Malaria, kisukari, magonjwa ya figo, kinga ndogo ya mwili na pia ujauzito. UTI inatibiwa kwa dawa za antibiotics na pia ukiwa msafi huwezi kupata UTI mara kwa mara. ************************************************************************************ 5. MAGONJWA YA VIUNGO VYA NDANI VYA UZAZI/PELVIC INFLAMATORY DIEASE (PID) Utangulizi: Mpenzi msomaji wa JITAMBUE Tanzania leo tunaangalia magonjwa yanayoathiri viungo vya ndani vya uzazi kwa wanawake. Kitaalamu magonjwa haya yanajulikana kama Pelvic Inflammatory Disease kwa kifupi PID. PID kawaida au mara nyingi inawasumbua au kuwashambulia wanawake kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo nchi yetu Tanzania. Zaidi ya asilimia 60 ya wanawake wanaohudhuria kliniki za nje za magonjwa ya akina mama (outpatient) wenye matatizo ya ugumba yaani walioshindwa kupata mimba au watoto wanasumbuliwa na PID. PID/Pelvic Inflammatory Diseae maana yake ni nini? PID inamaanisha maambukizi (yaani infection) yanayoathiri viungo vya ndani vya uzazi vya mwanamke. Maambukizi haya yanajumuisha maambukizi katika kuta za ndani za tumbo la uzazi yanayojulikana kitaalamu kama “endometritis”, maambukizi katika milija ya kusafirishia mayai yajulikanayo kitaalamu kama “salpingitis”, maambukizi katika sehemu inayotoa mayai ya mwanamke yaani ovaries maambukizi haya kitaalamu yanaitwa“oophoritis” na mwisho maambukizi katika eneo lote la viungo vya uzazi yaana kitaalamu pelvic peritoneum na parametrium; maambukizi haya yanaitwa “Parametritis”. Kwa mantiki hiyo, maambukizi haya yote yanajumuishwa katika tafsiri ya neno moja ijulikanayo kama “Salpingoophoritis”. Hata hivyo, maambukizi madogo (mild infection) yanaitwa Pelvic Inflammatory Disease (PID). AINA ZA PID Kwa kawaida yapo makundi mawili ya aina za PID yanayojulikana kama “Primary” na “Secondary”.
Maambukizi katika milija usababisha kukusanyika kwa maji (oedema) na usaha au maji maji meupe kama usaha. Hii hali usababisha maambukizi makali ambayo uweza kutengeneza jipu baada ya kusambaa katika fumbatio la viungo (peritoneum) ambapo jipu hili uitwa “pelvic abscess”. Hapa mgonjwa upata maumivu makali sana chini ya kitovu au kinene, upata homa kali sana, maumivu wakati wa kukojoa. Kumbuka: Kisonono au gonorrhea unakipata kwa njia ya kujamiana.
Madhara haya yanaweza kutokana na:
Maambukizi katika madhara haya mara nyingi ni bakteria wanaotokana na choo/kinyesi. Bakteria hawa wanajumuisha E. Coli, Klebsiella, Salmonella, Proteus vulgaris, peptostreptococcus na streptococcus. Utatambuaje kuwa una PID?
Ushauri: Ukiona dalili hizi nenda kituo cha afya ukamuone daktari ili aweze kukupatia tiba sahihi kwani PID inasababisha ugumba usipotibiwa vizuri na kupona kabisha.
Kawaida matibabu yanategemea na ukubwa wa tatizo. Ukubwa wa tatizo umegawanywa katika makundi makuu matatu:
Kundi la kwanza na la pili yanatibiwa kwa kupewa dawa/tiba na mtaalamu wa afya hususan daktari. Kundi la tatu yaani Chronic PID mara nyingi tiba yake ni dawa za kupunguza maumivu na pia kupata ushauri wa daktari. Hakuna dawa unayoweza kupewa ili tatizo hili liondoke au liishe badala yake unatuliziwa maumivu tu. Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa basi upasuaji (surgical intervention) unaweza kutumika kama njia ya tiba. Madhara ya PID PID isipotibiwa vizuri na kupona inaweza kuathiri afya ya mwanamke kimwili, kijamii na kisaikolojia. Mgonjwa anaweza kuishia na kupata ugonjwa sugu yaani “chronic PID” ambayo uweza kumsababishia maumivu makali wakati wa kujamiana na pia kupata matatizo ya mzunguko wa hedhi. Na pia inaweza kusababisha jibu na pia maambukizi katika fumbatio la viungo vya ndani yaani “severe peritonitis” ambayo ni hatari kwa maisha. Pia inaweza kuishia kutengeneza uvimbe katika milija na ovari yaani “Tubal Ovarian Masses TOM”. Hii inaweza kupelekea kupata ugumba wa muda yaani “sub fertility” au ugumba wa kudumu yaani “infertility”. Haya madhara umsababishia mwanamke kuathirika kijamii na kisaikolojia na pia umletea msongo wa mawazo. Talaka, kutengana na hata kujiua (suicide ) ni matokeo ya kijamii na kisaikolojia ya PID. Hitimisho: PID ni sababu kubwa ya kusababisha madhara kwa wanawake. Inasababisha madhara si tu kwa wanawake na pia kwa jamii nzima. Ina madhara kimwili, kijamii na kisaikolojia. ************************************************************************************* 6. UVIMBE KATIKA TUMBO LA UZAZI/FIBROIDS Utangulizi: Uvimbe katika tumbo la uzazi la mwanamke ukiondoa mimba kawaida ujulikana kitaalamu kama “pelvic tumour in women”. Uvimbe huu utengenezwa na tishu za misuli ya tumbo la uzazi ambayo uitwa “Fibroids” au “Fibromyoma” au “Uterine Myoma”. Mara nyingi uvimbe wa aina hii uanzia 5 hadi 30 kwa namba. Ufanana kama umbo la yai au kiazi ulaya na huwa na nundu nundu yaani “lobulated surface”. Uvimbe huu huwa mgumu (Hard). Sababu:
Ni mara chache wanawake chini ya miaka 20 kupata uvimbe katika tumbo la uzazi. Mara nyingi huwapata wanawake wenye umri kati ya miaka 35 hadi 45. Wanawake ambao hawajapata uzao au kuzaa (nulliparous) au wenye ugumba. Kawaida huwapata wanawake wa jamii ya watu weusi na pia hutokea katika familia. Maeneo ambayo uvimbe utokea: Mara nyingi uvimbe utokea maeneo yafuatayo:
Dalili:
Uvimbe unaweza kugunduliwa vipi?
Madhara ya Uvimbe huu (fibroids)
Matibabu:
Upasuaji upo wa aina mbili:
Ushauri: Hili tatizo uwapata sana wanawake wenye umri kati 35 na 45, wanawake ambao hawana watoto. Hivyo ninawashauri wanawake wajitahidi kupata ujauzito kabla ya kufikia miaka 35 ili kuondokana na hatari ya kupata uvimbe huu. ************************************************************************************* 7. TATIZO LA UGUMBA (UTASA) /INFERTILITY Maana ya Ugumba/Utasa Ugumba ni kushindwa kupata mimba /ujauzito baada ya mwanamke kukutana kimwili/kujamiana/kufanya tendo la ndoa na mwanaume kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja) bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. Pia ugumba ni kushindwa kwa mwanaume kutungisha au kumpa mimba mwanamke baada ya kukutana nae kimwili/kujamiana nae au kufanya nae tendo la ndoa kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja) bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. Hivyo ugumba unatokea pande zote mbili yaani mwanaume na mwanamke. Watu wengi ufikiri kuwa ugumba ni kwa mwanamke peke yake. La hasha! Ugumba pia uwapata wanaume kwa kushindwa kutungisha mimba kama tutakavyoona kwenye sababu za ugumba. Aina za Ugumba/Utasa Ugumba umegawanyika kitaalamu katika makundi makuu mawili: a) Ugumba wa asili/wa kwanza (Primary Infertility): Hapa hakuna mimba au ujauzito uliowahi kutokea kwa kipindi cha miezi 12 ya kujamiana au kufanya tendo la ndoa bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. b) Ugumba wa pili (Secondary Infertility): Kushindwa kupata mimba au ujauzito baada ya mimba ya kwanza au zaidi. Hii ina maana kwamba mwanamke amewahi kupata mimba au kuzaa mtoto mmoja au wawili lakini sasa anashindwa kupata mimba nyingine. Pia mwanaume wamewahi kutungisha mimba au kumpatia ujauzito mwanamke lakini sasa hawezi tena kumpatia ujauzito. Jinsi tatizo linavyoathiri/Incidence Karibu asilimia 15 ya wanandoa ni wagumba au tasa. Kiwango kikubwa cha magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana katika jamii usababisha zaidi tatizo la ugumba au utasa. Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana ni kama:
Utambuzi wa ugumba / Utagunduaje kuwa una ugumba? Kama nilivyoeleza hapo awali katika maana ya ugumba dalili kuu ya ugumba ni kutopata mimba au ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja kama hutumii njia yoyote ya uzazi wa mpango. Hivyo ukiwa na hali hiyo ni vema kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi wa kuweza kubaini tatizo ni nini? Kwa kawaida sababu za ugumba kwa wanaume uchangia asilimia 30, mwanamke asilimia 40 na asilimia 30 hutokea kwa pande zote mbili yaani mwanaume na mwanamke. Hivyo ukiwa na tatizo hili katika ndoa yako ni vema mwende kumuona daktari wa magonjwa ya akina mama ili aweze kuwafanyia uchuguzi zaidi na pia kuwapatia ushauri jinsi ya kupata mtoto. Sababu za Ugumba kwa Mwanaume Mwanaume anaweza kushindwa kutungisha mimba au kumpatia ujauzito mwanamke kwa sababu zifuatazo:-
Haya yote yanaweza kutambuliwa na wataalamu wa afya tu baada ya kukufanyia uchunguzi wa kitaalamu hivyo ninakushauri kama unatatizo hili uende kumuona daktari ili akusaidie kugundua tatizo liko wapi. Sababu za Ugumba kwa Mwanamke Kama nilivyoeleza awali mwanamke anachangia asilimia 40 katika tatizo la ugumba katika ndoa. Sababu za ugumba katika mwanamke zinaweza kuwa kama ifuatavyo:
Sababu za ugumba kwa pande zote mbili
Ni vizuri kumuona daktari ili aweze kuwasaidia kutambua lini yai la kike linakuwa limekomaa tayari kwa kutungishwa ili tarehe zinapokaribia basi mnakutana kimwili. Vipimo. Vipimo vipo kwa ajili ya Mwanamke na Mwanaume. Vipimo kwa pande zote mbili
Vipimo kwa Mwanaume
Vipimo kwa Mwanamke
Matibabu Vipimo vinavyofanyika ni kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo na pia ni tiba. Kwani tatizo likishagundulika ni nini na likatibiwa basi ujauzito hupatikana. Asilimia kati 15 hadi 20 ya wanandoa wenye tatizo la ugumba wanaofanyiwa uchunguzi wa kitaalamu upata uzazi (mimba). Hivyo ninawashauri wale wote wenye tatizo la ugumba kwenda kuwaona madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama ili waweze kuwasaidia kupata watoto. ************************************************************************************** 8. UGONJWA WA MALARIA Malaria ni nini? Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea (mdudu) kinachonyonya damu ya binadamu. Kimelea hiki kinajulikana kama “parasite”. Lakini watu wengi uelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Kuna aina nne ya vimelea (parasites) vinavyosababisha malaria navyo ni:
Kimelea ambacho ni hatari na kina madhara makubwa kwa binadamu ni Plasmodium Falciparum. Plasmodium Vivax hakina madhara makubwa ingawa kimesambaa sana kuliko kile cha Falciparum. Plasmodium Falciparum husababisha vifo kwa haraka. Kimelea cha malaria hubebwa au uishi katika utumbo wa mbu jike aina ya Anopheles. Jinsi gani mtu anapata maambukizi ya vimelea vya malaria?
Makundi gani ya watu huathirika sana na ugonjwa wa malaria?
Kwa nini malaria ni muhimu?
Mzigo utokanao na ugonjwa wa Malaria
Malengo ya Millenia Lengo 1: Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa Lengo 2: Kufikia elimu ya msingi kwa wote Lengo 3: Kukuza usawa, jinsia na kuwawezesha wanawake Lengo 4: Kupunza vifo vya watoto wadogo kwa asilimia 20% barani Africa Lengo 5: Kupunguza vifo vya mama wajawazito hususani vinavyotokana na malaria Lengo 6: Kupambana na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine. Lengo 7: Kuhakikisha mazingira endelevu Lengo 8: Kuendeleza ushirikiano wa maendeleo kimataifa Malengo ya Milllenia yanayolenga Malaria ni Lengo 1: Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa Lengo 4: Kupunza vifo vya watoto wadogo kwa asilimia 20% barani Africa Lengo 5: Kupunguza vifo vya mama wajawazito hususani vinavyotokana na malaria Lengo 6: Kupambana na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine. Mpango wa kuzuia au kupambana na Malaria Historia inaonesha kuwa kwenye miaka ya 50 (1950s) kulikuwa na mpango au mkakati wa kutokomeza malaria ulimwengu mzima. Kwa matokeo hayo ya mpango huo, malaria ilitokomezwa takribani nchi nyingi duniani. Mwaka 1969 Mpango huu au mkakati huu ulisitishwa kwa sababu zifuatazo:-
Hivyo Mpango au mkakati wa kutokomeza kabisa malaria ulibadilishwa na kuwa Mpango wa Kuzuia Malaria. Kipindi cha Miaka ya 70 (1970s) na 80 (1980s) malaria haikupewa kipaumbele au umuhimu. Mpango wa Kuzuia Malaria Hali halisi ya sasa:
Roll Back Malaria Mpango huu ulizinduliwa rasmi mwaka 1998 lengo likiwa ni kupambana na Malaria barani Africa. Mashirika yaliyokubaliana kushirikiana katika mpango huu ni WHO, UNDP, UNICEF, na WB (Benki ya Dunia). Lengo kuu ni kupunguza mzigo au tatizo la Malaria ifikapo mwaka 2010. Mikakati iliyowekwa kufikia lengo hili ilikuwa:-
Tatizo la Malaria Duniani (Ulimwenguni) Mwaka 2012 wagonjwa wa malaria walikadiriwa kufikia milioni 219.
Mwaka 2012 vifo vilivyotokana na ugonjwa wa malaria vilikadiriwa kufikia laki sita na elfu sitini (660,000). Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo na Nigeria ilichangia 40% ya vifo vyote. 85% ya vifo barani Afrika walikuwa watoto chini ya miaka 5. 5% ya vifo hivyo ilikuwa watoto chini ya miaka 5 kutoka Kusini Mashariki ya Asia. Nchi zilizo na maambukizi au tatizo la malaria ni 104. Maambukizi ya malaria yanaendelea kwenye nchi 99. Mpango wa kuzuia Malaria upo katika nchi 79 Mpango wa awali wa kuondoa malaria (Pre-elimination phase) upo katika nchi 10 Mpango wa kuondoa malaria (Elimination Phase) upo katika nchi 10 Prevention and Reintroduction phase nchi 5 Malengo Nchi 50 (9 barani Afrika) kupunguza maambukizi mapya ya malaria kwa 75% ifikapo 2015 Nchi 4 kupunguza kwa asilimia kati ya 50 na 75. Haja mahususi kwenye nchi 41 zenye maambukizi kwa asilimia 85. Uchunguzi wa vimelea, ugonjwa na matibabu yake. Kwa kawaida mtu akishaambukizwa vimelea vya ugonjwa wa malaria; vinachukua muda wa nusu saa (dakika 30) kusafiri hadi kufika kwenye ini lako. Vikifika kwenye ini vinaanza kuzaliana kwa wingi na hatimaye vinaingia kwenye mzunguko wa damu yako na hapo ndipo vinaanza kutafuna seli nyekundu ya damu yako. Vikiwa kwenye damu ndipo mtu anajisikia dalili za kupanda na kushuka kwa homa, kutetemeka mwili. Dalili za Malaria Dalili za malaria zinategemea mtu na mtu kutokana na nguvu za kinga yake. Hata hivyo dalili zinazowapata wagonjwa wa malaria ni zifuatazo:-
Kumbuka: Hizi dalili pia utokea katika magonjwa yanayoambukizwa na bakteria mfano Homa inaweza kuwa dalili ya UTI, Pneumonia, Typhoid. Kukooa kunaweza kuwa sababu ya maambukizi katika mapafu mfano pneumonia, kifua kikuu n.k Kutapika na kuharisha inaweza kuwa dalili za magonjwa ya maambukizi ya tumbo pia. Hivyo ni vema ukipata dalili hizi usichukue dawa bila kupata uchunguzi wa kitaalamu na pia ushauri kutoka kwa madaktari. Unapopata dalili hizi wahi hospitali ili wataalamu wakuchunguze na kujua ni ugonjwa gani ulionao. Matibabu ya malaria: Matibabu yanatolewa kulingana na aina ya malaria uliyonayo. Kuna aina mbili za malaria
Malaria isiyosugu tunatumia dawa ya Mseto (ALU) na mgonjwa anatumia dawa akiwa nyumbani kwake Malaria sugu tunatumia dawa ya Quinine kwa njia ya dripu na mgonjwa anapatiwa matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya. Mgonjwa analazwa hospitalini hadi anapopata nafuu na kuweza kula mwenyewe. Ushauri: Kama tulivyozungumza malaria ni ugonjwa hatari unaoua kwa haraka hivyo ninawashauri pindi unapohisi una dalili tulizozizungumza hapo awali, wahi katika kituo cha kutoa huduma za afya kilichokaribu na wewe ili upatiwe uchunguzi na kupata tiba sahihi. Usitumie dawa bila kumuona daktari kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unaongeza usugu wa dawa mwilini mwako bila sababu ya msingi na pia unahatarisha maisha yako. ************************************************************************************** 9. UGONJWA WA SARATANI Saratani ni nini? Saratani hutokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na hivyo kutokuwa katika hali yake ya kawaida. Seli hizo hukua na kuongezeka bila utaratibu maalum na huweza kusababisha uvimbe. Seli hizi huweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kwa mfumo wa damu au limfu (lymph). Sehemu gani za mwili saratani huweza kutokea? Saratani huweza kutokea sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo matiti, koo, mapafu, kinywa, utumbo mpana, shingo ya kizazi, ovary, tezi ya kiume (prostate), ini, ngozi na damu. Watu wangapi wanakadiliwa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa saratani? Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadilia ifikapo 2030 vifo vitokanavyo na ugonjwa wa saratani itakuwa milioni 12 ikilinganishwa na mwaka 2005 ambapo vifo vitokanavyo na saratani vilikuwa milioni 8. Hivyo kutakuwepo na ongezeko la kiasi cha milioni 4. Hii itakuwa ni idadi kubwa sana ya vifo ikilinganishwa na magonjwa mengine kama malaria, Ukimwi, Kifua Kikuu, vifo vya watoto wachanga, ajali za barabarani, maambukizi ya kifua, kiarusi, na magonjwa ya moyo. Inakadiliwa ifikapo mwaka 2030 idadi ya vifo vitokanavyo na malaria itakuwa chini ya milioni 2. Idadi ya vifo vitokanavyo na Ukimwi na Kifua Kikuu pia vitapungua na vitakuwa milioni 2 kwa ugonjwa wa Ukimwi na chini ya milioni 2 kwa kifua kikuu. Wakati huo huo vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na kiarusi vitakuwa vinaongezeka sambamba na saratani. Vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo vitakuwa milioni 10 wakati vifo vitokanavyo na kiarusi vitakuwa milioni 8 ifikapo 2030. Kwa hiyo tunaweza kuona jinsi gani saratani inavyozidi kusababisha madhara kwa binadamu hususan wa kizazi kipya. Inakadiliwa pia kutakuwepo na ongezeko la wagonjwa wapya wa saratani katika nchi zinazoendelea ikilinganishwa na nchi zilizokwisha endelea ifikapo 2020. Wagonjwa wapya kwa mwaka wanakadiliwa kuwa milioni 9 katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wakati wagonjwa wapya katika nchi zilizoendelea itakuwa chini ya milioni 6 kwa mwaka. Hii inahashiria kwamba saratani itakuwa inaongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo kuna haja ya kuchukua tahadhari kukabiliana na tatizo hili ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na kuongezeka kwa ugonjwa wa saratani. Kuzuia saratani ndo jibu sahihi katika nchi zetu zinazoendelea. Inakuwaje mtu anapata saratani/Saratani inatokeaje? Kwanza kabisa tujue jinsi gani saratani inavyotokea. Hatua za Saratani:-
Changamoto za kuzuia Saratani Baadhi ya njia au mbinu za kuzuia saratani hazitokani kabisa na njia za utoaji huduma za afya au elimu ya afya kwa umma. Mfano:-
Tufanye nini ili kupunguza uwezekano wa kupata saratani
Hatua za awali za kuzuia saratani (Primary cancer prevention)
Hatua za pili za kuzuia saratani (Secondary cancer prevention)
Uchunguzi wa matiti Uchunguzi wa mapafu Uchunguzi wa tezi la kiume Uchunguzi wa utumbo mpana Na pia hatua zote za awali za kuzuia saratani Hatua ya tatu ya kuzuia saratani (Tertiary Cancer Prevention)
************************************************************************************** 10. MAGONJWA YA KURITHI KUTOKANA NA NDUGU WA DAMU KUOANA Nini madhara ya kiafya yatokanayo na ndugu wa damu au wajomba kuoana? Kwa kawaida binadamu wana nakala (copy) mbili za jeni yaani sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani inayoitwa kitaalamu “XY sex Chromosome”. Watu wengi kwenye jamii asilimia 99% wana nakala mbili za jeni zilizona afya nzuri yaani (“Healthy D gene”) DD. Asilimia 1%, wana jeni moja yenye ugonjwa ambayo kitaalamu inaitwa (“One copy of the diseased gene”) Dd. Jeni iliyo na ugonjwa inaitwa “Recessive”. Jeni hii iko kwa mama (mwanamke). Jeni isiyo na ugonjwa iko kwa baba ambayo uitwa “Dominant gene”. Kwa kawaida watu wana afya nzuri isipokuwa wakiwa na jeni mbili zenye ugonjwa yaani “diseased gene” (dd). Iwapo mama yako amebeba nakala moja ya jeni (Dd) iliyona ugonjwa, basi unakuwa na asilimia 50% ya kurithi hiyo jeni na pia watoto (siblings) utakaowapata watarithi hiyo jeni. Ukioa mwanamke au kuolewa na mwanaume yeyote kwenye jamii ambaye hamna uhusiano wa kuzaliwa pamoja (hapa tunaongelea ile asilimia 1%, una asilimia 0.5% yakupata jeni yenye ugonjwa. Kama unaoa ndugu yako, uwezo wa kupata jeni yenye kasoro (ugonjwa) itaongezeka hadi kufikia asilimia 25%. Kwa hiyo kama mtu atamuoa ndugu yake bado asilimia ni ndogo ya kupata jeni iliyo na ugonjwa. Lakini ukizidisha asilimia ya kuwa na jeni iliyona ugonjwa; hivyo itaongezeka na kuanza kuwa na hofu. Kawaida watu wanaooana ndugu kiwango cha kuenea kwa jeni yenye ugonjwa ni mara mbili zaidi ya watu wasio ndugu. Ndugu wa baba na mama mmoja ni asilimia 50% ya kuwa na jeni ya ugonjwa. Wajomba (cousin) ni asilimia 12.5%. Magonjwa ya kurithi:-
Ndoa za ndugu katika jamii yetu: Kutokana na Sheria ya Ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1971 (The Law of Marriage Act, Reversed Edition 2002) kifungu cha 14 kinakataza ndoa za ndugu wadamu kuoana. Pia baadhi ya dini hususan za Kikristu zinazuia ndoa za aina hii. Baadhi ya madhehebu mengine yanaruhusu ndoa za aina hii. Lakini madhehebu haya sidhani kama yapo katika nchi yetu. Lakini ndoa za aina hii zimekuwa zinatokea sana katika familia za kifalme maeneo kama:
11. MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA KUANZA HEDHI Maumivu wakati wa hedhi kitaalamu hujulikana kama “Menstrual cramps” au “Dysmenorrhea” au “Period Pains”. Ni maumivu ambayo wasichana ujihisi chini ya kitovu na huzitokeza kabla ya kuanza hedhi na pia wakati wa hedhi. Wakati wa kupata hedhi, msichana huwa na mabadiliko katika via vyake vya uzazi. Ukuta wa mfuko wa uzazi, ambao umehifadhi damu ulikuwa tayari kupokea mimba humomonyoka kama yai halikurutubishwa. Damu ndani ya mfuko wa uzazi hufanya misuli ya mfuko huo kujikamua ili damu itoke nje. Kujikamua huku kwa kizazi ndiyo kunasababisha hayo maumivu na wanawake wengi huwa na maumivu kama haya. Aina ya maumivu wakati wa hedhi: Kuna aina mbili za maumivu wakati wa hedhi.
Nani hupata maumivu wakati wa hedhi? Karibu nusu ya wanawake wote hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu 15% ya wanawake hueleza kupata maumivu makali wakati wa hedhi. Imeonekana pia kuwa wanawake wasiofanya mazoezi hupatwa na maumivu wakati wa hedhi. Mambo mengine hatarishi yanayohusishwa na maumivu wakati wa hedhi ni kama:
Nini husababisha maumivu wakati wa hedhi? Kila mzunguko wa hedhi, kama hakuna mbegu ya kiume ya kurutubisha yai la kike, ukuta wa mfuko wa uzazi, ambao umehifadhi damu iliyokuwa tayari kupokea mimba humomonyoka kama yai hilo halikurutubishwa. Damu ndani ya mfuko wa uzazi hufanya misuli ya mfuko huo kujikamua ili damu itoke nje. (the uterus contracts to expel its lining). Kujikamua huku kwa kizazi ndiyo kunasababisha hayo maumivu na wanawake wengi huwa na maumivu kama haya. Hatua hii huchochewa na hormone zenye vitu vijulikanavyo kama “Prostaglandins” ambavyo huhusishwa na maumivu haya na pia maambukizi katika hatua za juu. Pia vitu vingine ambayo hujulikana kama “Leukotrienes”hutolewa kwa kiasi kikubwa wakati wa hedhi na hivi husababisha maumivu wakati wa hedhi. Nini dalili za maumivu wakati wa hedhi? Dalili za hedhi ni:
Utatambuaje kuwa una maumivu wakati wa hedhi? Mara nyingi wanawake hujitambua kuwa na maumivu wakati wa hedhi hata bila msaada wa Daktari. Kama ni mara ya kwanza inaweza kuwa vigumu kujitambua na hivyo kukulazimu kwenda kumuona daktari na pia kama unahusisha maumivu hayo na tatizo lolote la kiafya. Hapa Daktari anaweza kukusaidia kutambua kama maumivu haya ni maumivu yanayotokana na mabadiliko katika mzunguko wa hedhi au maumivu yanatokana na tatizo la kiafya. Matibabu ya maumivu wakati wa hedhi. Maumivu wakati wa hedhi hutibiwa na dawa zinazojulikana kama “Anti-prostaglandins” ambazo hupunguza maumivu katika kuta za mfuko wa uzazi na kufanya hedhi kutoka nyepesi na kukupatia nafuu. Mfano wa dawa hizi ni Ibuprofen au naproxen. Wakati mwingine Daktari anaweza kutoa vidonge vya uzazi wa mpango ili kuzuia kukua au kukomaa kwa yai la kike na hivyo kupunguza maumivu wakati wa hedhi. Unawezaje kuepuka na maumivu wakati wa hedhi? Unaweza kuepuka maumivu wakati wa hedhi kwa kufanya yafuatayo:
Ushauri: Iwapo maumivu yatakuwa makali sana nap engine kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kuendelea na hedhi kwa siku zaidi ya sita; basi hii ni dalili ya kuwa na tatizo la kiafya. Ninakushauri umwone mtaalamu wa afya kwa uchunguzi na tiba. 12. TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE/ VAGINAL ITCHING UTANGULIZI Nimekuwa nikipokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa wapenzi wasikilizaji wa kipindi chetu cha “IJUE AFYA YAKO” wengi wakilalamika kusumbuliwa na muwasho sehemu za siri. Ninapenda kutumia fursa hii kuwaelimisheni kwa ujumla kwani maswali yamekuwa yakifanana. Leo katika kipindi chetu cha Ijue Afya Yako tutaongelea tatizo la kuwashwa sehemu za siri kwa Wanawake. Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi na maambukizi mengine ya bakteria watokanao na kujamiana. Wakati mwingine alegi pia inaweza kusababisha mwasho. Muwasho maeneo ya ndani ya uke au kwenye mashavu ya uke husababishwa na mambo mengi. Muwasho ndani ya uke (vagina) unaweza kutokana na matumizi ya kemikali, sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria ( detergents or soaps), kuosha ndani ya uke na sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu tunasema vaginal douching) kitendo hiki husaidia kuua bakteria wanaoishi kwenye uke (normal flora) kwa ajili ya kuulinda, kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers), sabuni za bafuni (bath products), madawa ya usafi kwa akina mama (feminine hygiene products) na njia za uzazi wa mpango. Wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata mwasho kutokana na kubadilika kwa kiwango cha homoni ya Oestrogen. Kwa kipindi hiki kuta za uke huwa nyembamba na kukauka na hivyo kupelekea kupata mwasho. NAMNA GANI TUNAWEZA KUZUIA MWASHO SEHEMU ZA SIRI? Wanawake wanatakiwa kuchukua hatua zifuatazo kuzuia mwasho sehemu za siri:
13. UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI/VAGINAL CANDIDIASIS Fangasi za ukeni ni nini? Fangasi za ukeni hujulikana kama Candida. Na zile zinazosababisha ugonjwa ukeni zinajulikana kama Candida Albicans. Fangasi hawa husababisha mwasho mkali sana, uvimbe kwenye kuta za ukeni na pia mtekenyo. Fangasi hawa pia huweza kuambukizwa kwa njia ya kujamiana ingawa wengi hawazihusishi na magonjwa ya kujamiana. Unapataje fangasi hawa? Kawaida fangasi hawa kwa asili hupatikana kwenye maeneo ya ukeni. Lakini ukuaji wake huthibitiwa na bakteria wanaoishi ukeni wajulikanao kama “Lactobacillus”. Bakteria hawa huwafanya fangasi hawa wasikue lakini pindi bakteria hawa wanaposhindwa kufanya kazi vizuri basi fangasi hawa ukua na kuanza kusababisha madhara. Fangasi hawa hutibika kiraisi sana. Kama hunapata fangasi hawa mara kwa mara au wanarudiarudia basi inawezekana kuwa fangasi hao ni wa aina nyingine hivyo Daktari anahitaji kukufanyia uchunguzi zaidi wa kimahabara. Sababu nyingine zinazofanya mwanamke kupata fangasi za ukeni ni:
Dalili za Fangasi za ukeni
Namna ya kutambua Ugonjwa Ukienda hospitali Daktari atachukua maelezo yako namna gani tatizo hili limeanza na kama umewahi kuwa na shida kama hiyo hiyo na dawa ulizokwisha tumia na pia kama umewahi kupata magonjwa yoyote ya kujamiana. Kisha atakufanyia uchunguzi kwa kutazama sehemu zako za siri hususan kwenye kuta za uke na pia ndani kuona shingo ya uzazi. Kutokana na Daktari atakayoona anaweza kuamua kuchukua kipimo kwa ajili ya mahabara. Kipimo hiki kinaitwa “Vaginal Culture” Matibabu ya Fangasi za ukeni Matibabu yanategemea kiwango cha maambukizi pamoja na madhara ya ugonjwa a) Maambukizi madogo: Mara nyingi Daktari wako atakupatia dawa za kumeza kwa siku chache, kupaka au kuweka ukeni. Dawa hizi unaweza kutumia siku moja hadi tatu. Dawa zinazotumika ni kama Gynazole (Gynazle), Lotrimin, Monistat na Terazol. Dozi moja ya dawa ya kumeza inaweza kutumika mfano Diflucan Ushauri: Husitumie dawa yoyote bila kuandikiwa na daktari. Ukihisi una tatizo hili ni vema uende kituo chochote cha Afya kilichokaribu nawe ili umwone Daktari kwa matibabu na ufuatiliaji pindi tatizo linarudia katika kipindi cha miezi miwili. b) Maambukizi makubwa: Haya huhitaji matibabu makubwa zaidi. Ukiwa na dalili hizi ni vema ukamuone daktari:
Matibabu hapa yanaweza kuwa kama ifuatavyo:
Jinsi ya Kuzuia maambukizi ya Fangasi za ukeni. Ni vema kutambua nini kilikusabibishia kupata maambuki haya. Kwa mfano Wanawake wengine husema walipata maambukizi haya baada ya kutumia dawa za antibiotikisi. Ukitambua kitu kilichokusababishia tatizo hili basi unaweza kuzuia isitokee tena. Mambo mengine ya kusaidia kuzuia maambukizi haya ni:
|
Comments
Post a Comment