SABABU ZAKUTOYÀFIKIA MAFANIKIO


SABABU 20 ZITAKAZOKUFANYA USHIDWE KUYAFIKIO MAFANIKIO YAKO KATIKA MAISHA                      

Habari ndugu msomaji wa makala zangu, awali ya yote nikupongeze kwa kuendelea kufuatilia makala hizi, leo tutaanza mada yetu yenye kichwa cha habari hapo juu kwakuwa mada ni ndefu zaidi nitakuwa naikatisha ili kukupa muda wa kutafakari na kuyaweka kwenye matendo Yale ambayo tutakuwa tunajifunza pamoja, nakusihi uendelee kujifunza pamoja nami, tutajifunza pamoja sababu ambazo zitakufanya ushindwe kufikia mafanikio yako,kila mtu anatafsri yake katika mafanikio kwaiyo wewe utatumia kulingana na tafsiri yako. japo zipo nyingi lakini hizi ni miongoni mwao.

1.KUFATA HISTORIA YA FAMILIA
Moja ya sababu ambayo inawafanya watu wengi kushindwa kufanikiwa katika maisha ni kufata historia ya familia yake, asilimia kubwa ya sisi watanzania tumetoka familia masikini, zisizokuwa na elimu kubwa, sasa wapo watu na wao wamebeba historia za familia zao, ilimradi mtu kwao hakuna aliesoma basi na yeye amekata tamaa ya kusoma, ilimradi familia yake ni masikini basi na yeye anarithi umasikini, hii humepelekea mtu kuacha kutafuta fursa za kubadilisha maisha yake sababu ya familia, ngoja nikwambie kitu kuzaliwa masikini ni bahati mbaya lakini kufa masikini ni hiari yako, wewe unaweza kubadilisha historia ya familia yako kama ukiamua na wewe ukawa mkombozi wao.

2.KUKOSA UJUZI NA MAARIFA
        Sasa hapa naomba nieleweke Kuna tofauti kati ya elimu kuubwa na ujuzi na maarifa, unaweza ukakosa elimu kuubwa ya kwenda Chuo kikuu lakini ukawa na ujuzi mkubwa na maarifa ya kufikia mafanikio yako, ndio maana matajiri wengi duniani hawana elimu kubwa ya vyuo lakini wanaujuzi mkubwa na maarifa ya kufikia ndoto zao, elimu kubwa ni mpaka uende shule, ufike Chuo kikuu huko ndiko unakoipata na wengi wanashindwa kufika huko, lakini ujuzi na maarifa unavipata mtaani, kwa kuhudhuria semina mbalimbali za mafunzo, Kuna semina zinaendeshwa huko mtaani na zingine zinaendeshwa kwenye mitandao hata ya watsap, hata mimi semina zangu nyingi najifunza za kwenye mitandao kwa mfano mwezi uliopita nililipia laki moja kuhudhuria whatsap business school, nilijifunza mengi nikiwa nyumbani, unaweza kupata ujuzi na maarifa kupitia kujisomea vitabu mbali mbali vya watu waliofanikiwa na wewe ukapata mbinu mbalimbali za kufikia mafanikio yako sana.

3.KUKOSA MAKUSUDI MAALUM
         Hii pia ni moja ya sababu ambazo zinaweza kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako katika maisha, ngoja nikwambie kitu unapoanzisha kitu labda mfano biashara au kitu chochote utakutana na watu wengi sana watakukatisha tamaa, wapo wanakwambia huwezi, wengine watakwambia bora uache unapoteza muda, wengine watakwambia hiyo ni ngumu huwezi, kama huna makusudi maalum, kama hujui kwanini ulianzisha hicho kitu ni rahisi sana kukiacha utakapokatishwa tamaa, lakini Ukiwa na makusudi maalum ndio yatakuwa kama taa inayokuongoza kwenye mafanikio, nilipoanzisha biashara muda mwingine nilikutana na changamoto hadi nilitaman kuiacha lakini kila lilipokuwa linanijia pepo la kuacha najiuliza nimeshatimiza makusudi yangu jibu linakuja bado nakomaa hadi leo naendelea kusonga mbele.

4.KUAHIRISHA AHIRISHA MAMBO
     Duniani Kuna mabingwa wa kuahirisha mambo, unamwambia kitu anakwambia nitafanya kesho, biashara nitaanza kesho, kuhudhuria mafunzo kesho, moja ya sababu ambazo zitakufanya ufe Ukiwa masikini ni kuahirisha ahirisha mambo, wahenga wanasema liwezekanalo leo lisingoje kesho, kuahirisha mambo sio tu kutazika ndoto zako Bali na wewe mwenyewe, kesho haitafika hata siku moja, na Mungu anakanuni zake anapokupa fursa ya kukuonyesha wazo fulani halafu usilifanyie kazi analipeleka kwa mtu mwingine, halafu ipo siku utakuta Kuna mtu tayali kufanya kama ulivyofanya wewe, halafu utajiuliza imekuaje, nimewahi kukutana na baadhi ya vijana ambao ninawaonyesha fursa ya biashara ambayo mimi nilianzia mwanzo kabisa hadi kutoka kwenye ajira na kuwa mjasiriamali 100% nilichokuwa nashangaa baadhi ya vijana niliokuwa nakutana nao anakwambia mimi subiri kwanza nijipange niielewe kwanza hiyo biashara halafu nitakuja sasa swali nikiwa najiuliza huyu anasema subiri kwanza aielewe wakati haifanyi ataelewaje? Basi nabaki nacheka tu, hakuna mafanikio yanayokuja kwa mtu mwenye kuahirisha ahirisha mambo unapopata fursa leo ianze leo hata kama kwa mara ya kwanza utashindwa lakini utajifunza na utasongambele. Ukisema kesho ndio utaanza imekula Kwako.

5.KUTOKUWA KUWA TAYALI KULIPIA GHARAMA ZA MAFANIKIO YAKO
       Wapo watu wengi sana wanahitaji mafanikio lakini ni watu wachache wako tayali kulipia gharama za mafanikio yao, Kitu pekee ambacho ninapenda kukwambia leo wewe ambae umepata nafasi ya kusoma makala hii ni kuwa kama hauko tayali kulipia gharama za mafanikio yako ni kazi sana kufanikiwa kwenye maisha yako, hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi lazima ulipe gharama kwanza, gharama yaweza kuwa muda, maana unahitaji kutoa muda wako kujifunza,wapo watu hawawezi kusoma hii makala eti ni ndefu lakini sio kwamba ni ndefu Bali hawako tayali kulipia gharama za kujifunza, gharama inaweza ikawa jitihada lazima ukubali kutoka jasho mafanikio sio rahisi, gharama zinaweza kuwa pesa, kwamfano unataka kufanikiwa kupitia biashara lazima ukubali kutoa pesa yako kuhudhuria semina mbalimbali, kujisomea vitabu na kuwalipa wataalam wa ushauri wa biashara, kama huwezi kufanya hivyo sahau kuhusu mafanikio, usiwe mgumu lipia gharama za mafanikio yako ndio utayapata.

6.UOGA
        Uoga ni ugonjwa mbaya sana kwenye mafanikio, wahenga walisema UOGA WAKO NDIO UMASIKINI WAKO, watu ni waoga sana kufanya vitu vitakavyoleta mafanikio yao binafsi, kama hautakuwa risk taker hutafanikiwa, Kuna mtu anataka kuanzisha biashara fulani lakini anaogopa jirani yake, rafiki yake, mme au mke wake atamuonaje,maisha yako yako mikononi mwako acha kuangalia watu, Kuna mtu mwingine yeye hawezi kuanzisha kitu anaogopa kukataliwa, mwingine anaogopa kushindwa, mtu anajiuliza nataka kuanzisha biashara nikishindwa je, ngoja nikwambie kitu matajiri wote unaowaona duniani wameshindwa mara nyingi tu, kushindwa ndio kujifunza, unapotaka kuanzisha kitu unapokuwa umeona fursa fulani ianze bila kuogopa, utafanikiwa, akili ya mwanadam iko hivi unapoogopa kitu fulani yenyewe inakuketea sababu, mfano fikiria kama wewe unataka kuanzisha biashara halafu Unaogopa utaanza kusikia sauti ndani yako ikisemA, kwanza hauna muda, mtaji wenyewe mdogo hautafanikiwa, halafu mmmhh wewe huna elimu hutaweza, oooh mara bado unakazi nyingi ofisin zikiisha ndo utaanza, mmmhh mbona hiyo biashara yenyewe hujaona aliefanikiwa, hizi zote ni sababu tu za Uoga na mwisho wa siku hafanyi ulichotarajia kufanya na umasikini unaeendelea kukuandama.

7.KUTOKUWA NA MATARAJIO YA KUFANIKIWA
Ukiwa umekata tamaa kabisa ya kufanikiwa huwezi hata kupambana katika maisha yao, Kuna watu tayali wameshakuwa na matarajio ya kutofanikiwa, Kuna mtu utamsikia bwana eee sisi wengine ndio tuliumbwa masikini hatuwezi kufanikiwa, kama huna matarajio ya kufanikiwa labda kutokana na maisha nakutia moyo amka simama tena ndani yako Mungu kukuumba wewe ni mshindi hata kama huoni wapi pakuanzia nitafute takuonyesha pakuanzia.

8.MAZINGIRA UNAYOISHI
Moja ya sababu inayoweza kukufanya usifanikiwe katika maisha yako ni mazingira unayoishi, hebu fikiria unaishi kwenye mazingira ya vijana wasiopenda kaZi wao wanapenda kukaa vijiweni tu utafanikiwa? Hebu fikiria unakaa kwenye familia ambayo kaZi yao ni kukukatisha tamaa utafanikiwa? Ili uweze kufanikiwa unatakiwa kubadilisha hayo mazingira simaanishi uhame, mimi nilifanya hivi nilianza kujisomea vitabu vya watu waliofanikiwa kwaiyo nikawa nakosa muda mwingi wa kukaa vijiweni, pili nilianza kutafuta marafiki wanaonitia moyo na wenyefikra kama mimi hivyo nikawa nimetengeneza mazingira mapya, hata wewe kama unamawazo ya kufanikiwa nakukaribisha uwe rafiki yangu usiogope.

9.FIKRA HASI
Kuna watu fikra zao zinawaza kushindwa tu wanaishia kushindwa, Kuna watu wao wanawaza kupata hasara tu wanaogopa kuanzisha biashara, Ukiwa na fikra hasi ni kazi sana kufanikiwa katika maisha hayo, kubadilisha hayo ni kubadilisha fikra zako.

10.KUKOSA MAAMUZI SAHIHI
Katika harakati zangu za kila siku za kuwaonyesha watu fursa mbalimbali za kukomboa maisha yao nimekutana na baadhi ya watu nawaonyesha fursa halafu nawauliza uko tayali kuanza, jibu nilikuwa napata hili ngoja nikamshaurishe mme wangu, ngoja nikaongee na mke wangu, ngoja nikamwambie na rafiki yangu halafu nitarudi, wote hawa hakuna alierudi na maisha yao yako vile vile aheri ya jana, hebu jiulize wewe unaenda kuomba maamuzi kwa mtu ambae hakijui hicho kitu au alishafanya akashindwa unadhani atakupa jibu gani, hiyo ngumu huwezi, sasa na wewe kwasababu ni mvivu wa kufikiri umeshikiwa maamuzi unaacha unaendelea kufa masikini, hakuna anaejua uchungu wa maisha ulionao ni wewe mwenyewe jifunze kuwa na maamuzi yako mwenyewe.

Comments

Popular posts from this blog

GROUP (KUNDI) ZA DAMU NA TABIA ZAKE

TOFAUTI YA DHAMBI,MAKOSA NA UOVU.

Madini ya Zink na Ugumba