
Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni. Zifuatazo ni baadhi tiba ambazo ni rahisi kuandaa mwenyewe ukiwa nyumbani na hazina madhara kabisa kiafya. 1. CHAI YA KIJANI (GREEN TEA) Green tea ni tajiri wa polyphenol,ina antioxidant yenye nguvu sana ambayo itaondoa plaque kuenea kwenye meno yako. Polyphenols imeonekana kuzuia bacteria kukua katika mdomo.Kwahiyo kufyonza chai ya kijani husaidia kuondoa harufu chafu ya vitunguu. Spinach, chai ya rangi,apples na mushrooms pia nazo zina polyphenols, unaweza pia kutumia aina hii ya vyakula na kinywaji baada ya kujiona mdomo unatoa harufu iliosababishwa na mlo wako. 2. MATUNDA NA MBOGA FRESH Fiber-nyingi hupatikana kwenye matunda na mboga, husaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomoni (na ku...