Glory na mauamivu
Nimemsikiliza Glory... Nimemsikiliza zaidi ya mara moja... Najaribu kulitazama hili jambo kiundani zaidi, tunachokiona kwa Glory ni matokeo ya jambo fulani na sio chanzo cha jambo hilo! Huwezi kutatua tatizo kwa kushughulika na matokeo bali jambo hutatuliwa kwa kushughulika na chanzo! Chanzo cha haya yanayompata Glory ni nini? Kwanini yupo hivi? Tatizo ni yeye au ni wanaume anaokutana nao? Glory ni mtu wa aina gani? Ana marafiki wa aina gani? Amelelewa katika familia ya namna gani? Malezi yake yapo vipi? Alianza mapenzi katika umri gani? Je amewahi kuumizwa? Mapenzi kwake yanamaanisha nini,? Tukiweza kujibu nusu ya haya maswali tutapata mwanga kuhusu chanzo cha matatizo ya Glory. Kumwambia tu ajitahidi sio msaada anaouhitaji, Glory amekwama, anahitaji nuru na ukiona mtu anasema shida yake hadharani ujue imefika katika viwango vya juu.... Hakuna mtu anayependa kuyasema matatizo yake ila yakizidi vinywa hufunguka vyenyewe! Shida ya Glory ipo katika makuzi yake ni t...