AINA ZA MAUMIVU YA TUMBO
Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ya mbavu kulia yanaweza kusababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo, maambukizi kwenye mfuko wa nyongo Cholecystitis , uvimbe wa ini, jipu kwenye ini, saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo. Maumivu chini ya chembe ya moyo husababishwa na vidonda vya tumbo, kiungulia, saratani ya tumbo na saratani ya kongosho. Maumivu pembeni mwa kitovu husababishwa na mawe ya figo Kidney Stones, maambukizi ya figo, Pyelonephritis na maambukizi kidoletumbo Acute Appendicitis Maumivu chini ya kitovu huweza kusababishwa na maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID, vivimbe vya mji wa uzazi, mimba kuharibika na saratani ya kibofu cha mkojo. Sababu nyingine za maumivu ya tumbo ni utumbo kujiziba Intestinal Obstruction, utumbo kujisokota Volvulus, kula sumu na mzio wa chakula fulani au ugonjwa wa Crohn Crohn’s Disease, N...