TRA ruksa kutembea na polisi ukusanyaji kodi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameibariki Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwatumia TAKUKURU pamoja na Jeshi la Polisi wenye silaha za moto wakati wanapokwenda kukusanya mapato pamoja na kodi kwa wafanyabiashara ambao ni wanaodaiwa sugu. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni Mjini Dodoma, amesema ni sahihi kwa kikosi kazi hicho (task force) kutumika kwa kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara sugu wenye lengo baya la kutotaka kulipa madeni na badala yake hutoa rushwa. Mhe. Lema alitaka kusikia kauli ya serikali juu ya mfumo unaotumiwa TRA wa kusumbua na kuwatisha wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku huku ikiwa inadaiwa kuwa mamlaka hiyo hutumia Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza , Arusha na Mbeya. “Ni kweli kwamba tunacho chombo ambacho kinachowajibika katika ukusanyaji wa mapato na kodi kutoka kwa...