SOMO MUHIMU JIJUE
UJUMBE WA LEO Kuanza kuchepuka kwa mwanamke ndani ya ndoa, huanza kwa mwanaume, ukiwa mchepukaji, mke naye baadaye anaweza kuwa mchepukaji. Mwanaume unamwambia mkeo awe mwaminifu, je wewe mwaminifu? SIyo unamwambia yeye awe mwaminifu halafu kumbe una vimada kadhaa nje ya ndoa, sasa kwa nini yeye awe mwaminifu na wakati wewe siyo mwaminifu? Mwanaume anasema kwamba anataka kuoa mwanamke bikira, sawa, ni vizuri, lakini je, wewe ni bikira? Je hujawahi kufanya mapenzi? Kama ndiyo, basi oa bikira, ila kama umewahi kufanya mapenzi, sioni sababu ya kuoa bikira. Mwanaume unakwenda kuoga, ukisikia simu yako inaita chumbani, na mkeo yupo huko, tayari unaanza kuwa na wasiwasi, mpaka wengine wanatoka na mapovu bafuni kwenda kuwahi simu ili mke asijue nani anapiga. Kama hujajiandaa kuoa, kama hujamaliza mambo yako, kama kila demu unataka kugonga, nadhani endelea kwanza, ukishamaliza mambo yako ndiyo uoe kwani vinginevyo, ndoa itakusumbua tu. Kama hutaki kumwamini mkeo ndani ya ndoa, utamwamini nani ...