Posts

Showing posts from February, 2017

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The Essentials Of Business Etiquette

Image
Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wangu? ni matumaini yangu kuwa umeamka salama siku hii ya leo. Leo ni siku nyingine bora sana na ya kipekee kwetu hivyo tunaalikwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo. Rafiki, tumia muda wako vema kwa manufaa yako mwenyewe na dunia nzima. Karibu sana rafiki katika makala yetu ya leo ambapo leo nitakwenda kukushirikisha mambo muhimu niliyojifunza katika uchambuzi wa kitabu. Nitakwenda kukushirikisha mambo machache kati ya mengi kupitia kitabu hiki. Karibu tuanze pamoja hadi tamati ya somo letu la leo. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Barbara Pachter. Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha The Essentials of Business etiquette na Barbara Pachter ni kama ifuatavyo; 1. Jina ni muhimu sana. Kila mtu ana jina lake na amepewa jina ili atambulike yeye ni nani. Jina linatambulisha biashara ya mtu. Jina linabeba biashara au kitu unachofanya. Kama unamwita mtu jina lake mwite kiufasaha na siyo jina la utani. Mara nyingi pen...