Maradhi ya fizi na meno
Ni matumaini yangu mu wazima wa afya wapenzi wasikilizaji, na karibuni kujumuika nami katika makala nyingine ya Ijue Afya Yako. Wiki iliyopita tulizungumzia usafi wa kinywa, umuhimu wake na pia jinsi ya utunzaji wa fizi na meno. Bado tunaendelea kujadili suala hilo ambapo leo tutazunguzia maradhi mbalimbali ya fizi na meno na namna ya kuyazuia. karibuni. Aina za maradhi ya fizi na dalili zake Kupiga mswaki na kutunza meno sio suala gumu na iwapo tutapiga mswaki ipaswavyo pamoja na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno, tunaweza kuzua maradhi ya fizi na pia meno kuoza. Maradhi ya fizi husababishwa na utando kwenye meno unaotengenezwa na bakteria, ute na chembechembe nyinginezo zinazoganda kwenye meno. Kwa mujibu wa Taasisi ya Meno ya Marekani (ADA) iwapo utando katika meno hautaondolewa huwa mgumu na kuwa ugwagwa wa meno au tarter inayotumiwa na bakteria. Mchanganyiko wa utando na ugwagwa katika meno husababisha uvimbe kwenye fizi hali inayojulikana kitaalamu kama gingivitis. Ukoga w...