Posts

Showing posts from March, 2016

UWEZO WA KUGHAIRISHA(SUSPEND) MAMBO

Kati ya sifa kubwa unayotakiwa kuwa nayo ili uweze kufanikiwa kimaisha ni uwezo wako wa kughairisha (suspend) mambo yanayokupa raha kwa muda mfupi ili kujenga mambo yatakayokupa furaha kwa muda mrefu. Mwanzoni mwa 1960 Professor Walter Michael wa chuo kikuu cha Stanford alifanya jaribio fulani la tabia ambalo limekua marufu sana miongoni mwa wanazuoni wa sayansi ya jamii na saikolojia. Jaribia hilo linajulikana kama “Marshmallow Experiment”. Katika utafiti huu aliwajaribu watoto wadogo kama 100 wenye umri wa miaka minne na mitano. Aliwaweka katika chumba na akawawekea kila mmoja kipande cha mkate mtamu wenye chocolate. Kisha akawaambia "Kama nikirudi nikakuta haujala huu mkate nitakupatia kimkate cha pili, ila kama nikirudi nikakuta umeshakula sitakupatia kitu." Kisha akawaacha kwa dakika kumi na tano (15) wakiwa peke yao chumbani halafu akarejea. Aliporudi alikuta matokeo kama ifuatavyo: 1. Zaidi ya watoto 60 walibugia ile mikate baada tu ya yule Profesa kutoka. Yani alipof...